Poor Serikali ya Kikwete walisema UDOM ni mafanikio yake ataacha sifa kumbe Majengo yananyonyofoka... na kwanini anatumwa Nape?
Kuna picha za Slaa Bwenini
Tuesday, 24 May 2011
NA BASHIR NKOROMO, DODOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ili kulipatia ufumbuzi tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza kwenye baadhi ya majengo.
Chama pia kimewaagiza viongozi hao kukagua miundombinu ya majitaka katika baadhi ya maeneo chuoni hapo, ili ifanyiwe marekebisho na kuondokana na adha ya harufu mbaya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliagiza hayo jana baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua baadhi ya majengo ambayo yana nyufa. Majengo yenye nyufa ni ya
mabweni ya wanafunzi wa Shule ya Sayansi ya Jamii yaliyoko Block 2 na 3.
"Kujenga chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yanakuwa katika hali bora," alisema.
Nape alishangazwa na nyufa hizo katika majengo ambayo hayajatimiza hata miaka mitano tangu yalipojengwa, jambo alilosema ni la hatari kwa usalama wa wanafunzi.
Awali, Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Idris Kikula, akizungumza na Nape, alisema chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama za masomo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Profesa Kikula alisema chuo hicho kina wanafunzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Msumbiji, na kina walimu kutoka Russia, India, Kenya, Nigeria, Korea, Japan, Poland na Sweden. Alisema chuo kina uhaba wa walimu kwa kuwa wengi waliopo sasa ni wazee na wengine wanaugua magonjwa yanayoambatana na utu uzima.
Profesa Kikula alisema tatizo hilo limewafanya kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000. Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini zaidi ya 200 wapo masomoni ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.
Last Updated ( Tuesday, 24 May 2011 20:29
Tuesday, May 24, 2011
NAPE ATEMBELEA UDOM LEO, AAGIZA MAJENGO YENYE NYUFA YASHUGHULIKIWE HARAKA
CCM imewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ili kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la nyufa zilizoanza kuitokeza kwenye baadhi ya majengo.
Chama kimewaagiza pia viongozi hao kukagua hali ya miundombinu ya majitaka katika maadhi ma maeneo chuoni hapo ili ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inatuamisha maji kutoka katika majengo na kusababisha adha ya harufu mbaya kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazima,m wengine chuoni hapo.
Maagizo hayo yalitolewa leo, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kutembelea chuo hicho na kagua baadhi ya majengo ambapo alishuhudia baadhi ya majengo yakiwa na nyufa.
Majengo yaliyoonyesha kuwa na nyufa ni katiba mabweni ya wanafuzi wa Shule ya Sayansi na Jamii yaliyoko Block 2 na 3 ambapo alionyeshwa na wanafunzi wanaoishi katika mabweni hayo.
"Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yake yanakuwa katika hali bora", alisema Nape.
Nape alionyesha kushangazwa kwake kuona majengo ambayo hayajatimiza miaka mitano tangu kujengwa kwake, kuanza kupata nyufa jambo ambalo alisema ni hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaoishi katika majengo hayo.
Mapema akizungumza na Nape, ofisini kwake, Makamu Mkuu wa UDOM Profesa, Idrisa Kikula alisema, sasa chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama zao zote za masomo na Bodi ya Mikopo.
Profesa Kikula alisema, wakati chuo hicho kina wanafunzi pia kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji, Walimu wapo kutoka nchi za Russia, India, Kenya, Nigeria,Korea, Japan, Poland na Sweden.
Alisema, moja ya changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa walimu kwa kuwa waliokuwepo zamani wengi ni wazee au wanaugua magonjwa mbalimbali yanayoambatana na utu uzima.
Profesa Kikula alisema, changamoto hiyo ya uhaba wa walimu imesababisha chuo hicho kuendelea kupokea wanafunzi wasiozidi 20,000 tu, wakati kina uwezo wa kuwa na wanafunzi hadi 35,000.
Alisema, katika kukabiliana na changamoto hiyo, chuo kimeajiri vijana zaidi ya 300, lakini ili walimu zaidi ya 200 kati ya hao 300 wapo masomoni ndabi na nje ya nchi kwa lengo la kuwa na wahadhiri wasaidizi wengi.
Ziara ya Nape mjini Dodoma amabayo ilimalizika jana, ilianza Jumatatu wiki hii, ambapo alihudhguria sherehe za kuagwa wanafunzi wa UDOM wa mwaka wa tatu ambao ni makada wa CCM.
Posted by: Bashir Nkoromo at bashir-nkoromo.blogspot.com
SIASA ZINAPOINGIZWA NDANI YA MABWENI CHUO KIKUU CHA DODOMA
[CENTER
Wanafunzi wa Sayansi ya Jamii, Chuo Chadema walizopamba katika chumba chao namba 0388 kwenye chuo hicho leo
Upande mwingine wa chumba hicho pamepambwa kama unavyoweza kuona upande wa kushoto nembo za Chadema na Picha ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Slaa. Kwa mujibu wa sheria wanafunzi wa vyuo, sekondari na msingi hawaruhusiwi kuendesha siasa katika maeneo hayo, ingawa wanaruhusiwa kuwa wanasiasa nje ya chuo.
Jengo la Utawala UDOM
Posted by: Bashir Nkoromo