Vyombo vya habari vimetuonyesha katibu uenezi na itikadi wa chama cha mapinduzi (CCM) ndugu Nape Nnauye akiwa katika ziara ya kikazi pale University of Dodoma (UDOM).
Mambo aliyoyafanya ni pamoja na kukagua majengo na miundombinu ya Chuo lakini pia alitoa maagizo kwa uongozi wa chuo kurekebisha matatizo madogo madogo aliyoyabaini katika miundombinu. Pamoja na hilo alikutana na wanachuo wanachama wa CCM wa mwaka wa tatu wa sayansi ya jamii (nadhani ni graduates to be). Sina uhakika kama ukumbi waliotumia upo chuoni au ni nje ya chuo maana haukutajwa jina katika vyombo vya habari. Ninachojiuliza ni mipaka ya sheria ya siasa katika vyuo vyetu ikoje? au inaviongelea vyama vya upinzani tu?
Lakini kikubwa zaidi ni mamlaka ya katibu wa chama cha siasa kupewa mapokezi na utawala UDOM hali kadhalika kutoa maagizo kwa uongozi wa UDOM kama kwamba hatuna Mawaziri wanaohusika na vyuo vikuu..!! Hii inatoa picha ipi kiutendaji? ina maana ile semina elekezi bado haikuainisha inter-communication katika baraza la mawaziri na nje hadi kwa viongozi wa chama? Nini mahusiano kati ya udom na ccm?
Je, kweli tutegemee wahitimu mahili kutoka katika chuo hiki kinachoonyesha mahusiano na vyama vya siasa? hakina uwezo wa kupata mahusiano na vyuo vingine duniani?
Nadhani viongozi waandamizi wa CCM walioko humu wanisaidie kupata ufafanuzi wa ile ziara ili nitoe wasi wasi wangu wa kiutendaji na umahili wa UDOM.
source:
Je! Nape alistahili kutoa maaagizo kwa uongozi UDOM? - Wavuti