Nyuki hawajaingia kwenye Mzinga, nifanyeje?

Kabisa, huwa najitahidi kujizuia kusoma jf hasa maeneo uliyotaja.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Japo haitakiwi kucheka mwenzetu ana shida huyuu...
jf sio sehem salama kuingia wakati upo kwenye ibada au unavuka barabaraaa

Nishawahi fakamia karavatiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyuki kama viumbe wengine, hawapendi adui kwenye eneo analotaka kuanzisha makazi

Umeweka mizinga tangu Julai, kuna uwezekano hiyo mizinga imeshavamiwa na wadudu wengine kama buibui n.k. na wanaishi humo

Mazingira kama hayo nyuki hawawezi kuanzisha makazi

Kagua kila baada ya muda flani, usiweke mizinga halafu unaisusa ukisubiri asali
Nina Mzinga 10 nimeiweka shambani mwezi Julai 2019 hadi sasa nyuki hawajaingia. Nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina Mzinga 10 nimeiweka shambani mwezi Julai 2019 hadi sasa nyuki hawajaingia. Nifanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari,
Ningependa kufahamu umeweka wapi mizinga hii?,je pana kivuli cha kutosha?
nakushauri uifungue mizinga na usafishe vizuri ndani,kwani kunaweza kuwa na wadudu wavamizi-ifute vizuri kwa kitambaa kisafi na ikiwezekana na maji ila usiweke sabuni.Hakikisha mizinga yako inakauka vizuri kwenye jua.baada ya hapo hakikisha hamna matobo tofuti na yale ya upande mmoja wanapoingilia nyuki--kama yapo hakikisha unayaziba.
Tafuta majani ya mchaichai(lemongrass) au nta(wax au masega ya zamani) na usugue ndani ya mzinga wa nyuki.Kwenye matobo ya kuingilia nyuki hakikisha pia unasugua na majani ya mchaichai.
utakapoweka mizinga-hakikisha hujaiweka chini kabisa-pawe na support au kichanja,na isiwe kwenye sehemu inayoingiza upepo directly kwenye mashimo(kama ni jangwani au kwenye upepo mkali hakikisha unaweka wind breakers.Pia hakikisha mizinga yako haipo mbali na chanzo cha maji--unless unapanga kuwawekea(kibeseni cha maji karibu na hapo)
Kila la kheri na natumaini utatupa mrejesho hapa.
 
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom