Nyuklia zina ubabe; Teknolojia ya kuzuia madhara ya silaha za nyuklia italeta mapinduzi makubwa katika uwanja wa vita

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika vita ya uvamizi inayoendelea kufanywa na Urusi nchini Ukraine ilifikiriwa na wengi ungekuwa uvamizi rahisi ambao ungedumu siku chache na Putin angetimiza malengo yake kwa gharama ndogo na kwa muda mfupi lakini uhalisia haujawa hivyo, jeshi la Urusi lilikouwa linaonekana kuwa imara sana dhidi ya jeshi la Ukraine sasa limekwama na limedhihirika kuwa la kawaida tu katika vita vya moja kwa moja na wanajeshi wa Ukraine.

Urusi imeshudia vifo vya wanajeshi wengi wanaokadiriwa kuzidi 10,000 na uharibifu mkubwa wa vifaa vya kijeshi.

Kinachoendelea sasa Ukraine ni jeshi la Urusi kuangusha mabomu na makombora hovyo hovyo kutokea mbali kila mahali katika miji ya nchi hiyo waliyoshindwa kuichukua. Hii inasababisha mauaji makubwa kwa raia na kuigeuza magofu miji ya Ukraine.

Kwa udhaifu mkubwa ulionekna katika jeshi la Urusi ni wazi endapo NATO ikiongozwa na Marekani ingeingilia vita hii Urusi ingeondolewa Ukraine kwa muda mfupi ila NATO imechuka tahadhari kuingilia kati moja kwa moja kwa sababu Putin alikwisha tishia kutumia silaha za Nyuklia ikitokea hivyo.

Wakati wa vita vya Pili vya dunia Adolf Hitler alipambana sana wanasayansi wa Ujerumani waweze kutengeneza bomu la Nyuklia lakin Wamarekani walimuwahi na pia wakamuondoa kabisa kabla hajafanikisha hilo. Kama angefanikiwa mapema huenda utawala wake wa Ki-Nazi ungedumu miaka 1000 kama alivyokuwa akijigamba.

Taifa lolote linalokuwa na silaha za nyuklia kwa sasa linajihakikishia ubabe hata kama lina jeshi na uchumi dhaifu sana, mfano mwingine mzuri ni Korea Kaskazini. Ni wazi magwiji wa teknolojia za silaha na vita wa magharibi watakuwa wanaumiza vichwa kumaliza undava ulioletwa nao wenyewe katika uvumbuzi wao wa silaha za nyuklia.
 
Umenikumbusha 'Operation Paperclip' na 'Operation Osoaviakhim'.......
 
Russian invented the NUKES in their own way! They didn't copy from western but Indian and Pakistan they harvested a loat from western lab.

Mwizi mkubwa wa Technolojia ya Nukes ni Abdisalam From Pakistan, huyo jamaa ndio alikuwa Supplier wa documents na vifaa nyeti vya kiutafiti in Middle East.

Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa Kuna mwanasayansi wa kirusi aliewahi fanya kazi kwenye nukes reseach centre, Warusi walipambana kivyao wakaja na teknolojia yao kama ilivyo kwa vifaa vingi. Usisikilize sana propaganda za magharibi.

Inasemekana Urusi ndio wanabomu lenye nguvu mara mia ya lile la hiroshima, hivyo wapo mbele ya wamagharibi
Watu wavivu wa kufikiri ni sisi waafrika na warabu.Hatuna BOMU la Nukes hivyo wazungu hawatuogopi kwa lolote.
Huwa nashangaa sana kwa nini waafrika tumelala hivi wakati wakorea walishajiongeza na hakuna wa kuwatisha tena.

Let us make AU BOM!!

Kuhusu kulipua mabomu hio ndio njia sahihi ya kupigana town warambapo mpinzani anajificha kwenye majengo na kukushambulia, njia hio ilitumika Afghanstan, Chechnya, Syria na sasa Ukrain( Do you think bom were invented tk blast the forest ? Absolute no !)

Hakuna Taifa babe linaweza kupigana vita ya mjini(terorism war) hata USA kafeli Afghan,Libya, Iraq, Somalia nk.

Russia anauzoefu sana na staili ya hio vita, isitoshe Russia hapigani na Ukrain tu bali anapigaba na NATO( Indirctly) , mengine ni propaganda tu!

Kumbuka mwanzo wa vita Vyombo vya magharibi vilidai eti msafara wa kijeshi wa Russia umekwama na hawatafanikiwa kuingia Ukrain, ukweli ni kwamba walifanikiwa kuingia na kuteja miji mingi tu pamoja na msaada mkubwa wanaopewa Ukrain.

Kubomoa mji ni mafanikio ktk vita , yani we mji kubaki magofu unaona ni ushindi, what kind of wining is that?
 

little to nothing.
Jf siku HIZI!!
 
UKWELI MTUPU MKUU NGOJA WARUSI WEUSI WAFUASI WA RAISI KICHAA ASIEJITAMBUA WAJE KUKUSHAMBULIA😂😂😂

Warusi weusi wa Buza
USA ameshinda vita ipi Kwa mfano ? Afghan,Iraq nk ?
Urusi ashafanikisha mission yake ya kuivuruga Ukrain ili isijiunge NATO.
Ni hivi Urusi kaivuruga Dunia pumbavu za NATO.
Tunaisoma namba mpaka Sichimbi kwa mfumuko wa bei, jamba jamba ya Urusi si ya kitoto. Nyie naina mmevimbiwa mihogo.
 
Sasa mkuu vita ya afganistani, iraq unailinganisha na hii ya ukraine, ambayo ni ya nchi na nchi?hizo nyingine USA, alikuwa anapigana na makundi ya kikaidi yaliyoko kwenye nchi hizo, mfano iraq kumuondoa sadam huseni ilichukua muda gani?ulikuwa ni muda mfupi tu, shida ikawa ni kupambana na hao magaidi, ambao kuwatambua ni ngumu!!lakini hii ya ukraine ni rahisi tu .hata Urusi miaka ya nyuma alishakutana na hali hiyo huko afganistani, akaamua kuondoka tu.Ki ukweli urusi hakutegemea kama mission yake hii ingechukua muda wote huu kabla ya kuiteka nchi nzima!!na kama ukraine angekuwa na air defense nzuri, kuweza kuzibiti mashambulizi ya anga, .Ndio maana putin anatishia kutumia silaha za nyuklia!!!
 
Silaha za Nuklia ziligunduliwa kwa mara ya kwanza Marekani chini ya J. Robert Oppenheimer baada ya maandiko na nadharia Kisayansi kutoka kwa Albert Einstein, wengine wote waliofuata waliichanganya utaalamu wa wanasayansi wao na ule wa Marekani walioupata kwa njia mbalimbali ikiwemo wizi kutengeneza nyuklia zao. Invention ya kitu kimoja huwa mara moja tu.
 
Nakupongeza sana kwa jibu zuri kwa hawa mamburula sijui walikuwepo wapi wakati wa vita ya Syria, kwenye vita ya mijini ni lazima uondoe maficho ya adui sasa pale kuna kichaka na kwa taarifa yako raia ndio imekuwa nguzo kubwa kwa ukrain isingekuwa hivyo Urusi ingemaliza hesabu mapema sana kama adui anajificha kwenye majengo ungefanya nini zaidi ya kudondosha jengo hii vita urusi wanashinda na hao NATO watafyata na ndio mwisho wa ubabe wa maneno bila vitendo
 
Binadamu ameweza kufika mwezini na kutuma satellite maili milioni kutoka umbali wa dunia kuangalia nyuma miaka billion 13 iliyopita, ameweza kufikika teknolojia za AI, kwenye utabibu ameweza kupandikiza moyo.
Wewe huko buza kwa mpalange ndio bado uko kwenye haiwezekani.
hakuna suluhu ya kupambana na nuclear
 
Newton Raphson method kwenye numerical analysis ni kanunu moja iliogunduliwa na watu wawili bila ya kuwa na mawasiliano.
Rejea Chanjo ya korona kila nchi(Kampuni) iligundua chanjo kivyake bilaa ushirikiano na nchi Nyingine.
Rejea 5G kila kampuni inapita njia yake, Huawei walitangulia ila kampunu kubwa zote zinapita njia yao.
Rejea Quantum kompyuta hii ni teknolojia mpya ambayo kila nchi ina pita njia yake.
Kwa hio inawezekana vumbuzi ikafanyika bila kukopi nchi nyingine.
Nenda ugogo jinsi Russia walivyojipatia Nukes tech.
Jambo lingine ni kwamba kujua theory sio guarantee ya kuunda kitu halisi, ingekuwa hivyo waafrika wangeshaunda hilo bomu au wangeunda ndege, electroni chip nk.
Kuna vitu kadhaa
1.Technical know why
2.Technical know how
Hizi mbili ni za msingi katika uundaji wa kitu chochote kile, kujua why haikusaidiii kuunda kitu bila kujua how.
Mkuu Nuke tech ya USA ilitokana na Manhatan project ambapi jopo la wanasayansi walikaa pamoja kushauriana, lile jopo lilikuwa na watu race mbali mbali, hivyi basi hakuna credit kwa mzungu wala muislael wala nani.Ni tejnolojia ilioletwa na ushitikiani wa binadamu kama ilivyo teknolojia ya kompyuta(Hakuna mvumbuzi mmoja)
Nimewahi fuatilia kwa kina jinsi wrusi na mataifa mbali mbali yalivyopata nukes tech sikuona mahala wameiba hio tech kama wanavyotuhumiwa wachina, wahindi na pakistni.
Urusi inafanyaga mambo kivyake kumbuka hata IB M na Rocket sayansi ambazo ni muhimu ktk nukes misile mwamba mbobezi ni urusi.
Tusitake kuamini kila teknolojia chanzo ni Western.
 
Jeshi la Marekani liliingia Iraq kama Urusi wanavyoingia Ukrain hakuna tofauti yoyote ispokuwa ya kimipaka tu.
Hao unaowaita magaidi ni wanajeshi wa Iraq walioshindwa kipambaba na midege ya NATO hivyo kubadili mbinu na kuingia vita ya mjini.
Vita ya mjini ndio kimbilio la majeshi yasiokuwa na nguvu duniani.
Unaonekana kupokea propaganda za kimagharibi za neno gaidi na kujenga imani thabiti.
Watu wanaopambania nchi yao dhidi ta wavamuzi wewe unawaita magaidi una akili kweli wewe?
Ulitaka USA akivamia nchi atandikiwe mikeka aingia kwa raha mustarehe!
Urusi anapambana na kile alichopambana nacho USA ktk hizo nchi, kwa hio tuite askari wa Ukrain magaidi kisa wamebadili tactic kama walivyofanya Afghanstan dhidi ya USA ?
Marekani ndio gaidi namba moja duniani, kama huamini sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…