Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Katika vita ya uvamizi inayoendelea kufanywa na Urusi nchini Ukraine ilifikiriwa na wengi ungekuwa uvamizi rahisi ambao ungedumu siku chache na Putin angetimiza malengo yake kwa gharama ndogo na kwa muda mfupi lakini uhalisia haujawa hivyo, jeshi la Urusi lilikouwa linaonekana kuwa imara sana dhidi ya jeshi la Ukraine sasa limekwama na limedhihirika kuwa la kawaida tu katika vita vya moja kwa moja na wanajeshi wa Ukraine.
Urusi imeshudia vifo vya wanajeshi wengi wanaokadiriwa kuzidi 10,000 na uharibifu mkubwa wa vifaa vya kijeshi.
Kinachoendelea sasa Ukraine ni jeshi la Urusi kuangusha mabomu na makombora hovyo hovyo kutokea mbali kila mahali katika miji ya nchi hiyo waliyoshindwa kuichukua. Hii inasababisha mauaji makubwa kwa raia na kuigeuza magofu miji ya Ukraine.
Kwa udhaifu mkubwa ulionekna katika jeshi la Urusi ni wazi endapo NATO ikiongozwa na Marekani ingeingilia vita hii Urusi ingeondolewa Ukraine kwa muda mfupi ila NATO imechuka tahadhari kuingilia kati moja kwa moja kwa sababu Putin alikwisha tishia kutumia silaha za Nyuklia ikitokea hivyo.
Wakati wa vita vya Pili vya dunia Adolf Hitler alipambana sana wanasayansi wa Ujerumani waweze kutengeneza bomu la Nyuklia lakin Wamarekani walimuwahi na pia wakamuondoa kabisa kabla hajafanikisha hilo. Kama angefanikiwa mapema huenda utawala wake wa Ki-Nazi ungedumu miaka 1000 kama alivyokuwa akijigamba.
Taifa lolote linalokuwa na silaha za nyuklia kwa sasa linajihakikishia ubabe hata kama lina jeshi na uchumi dhaifu sana, mfano mwingine mzuri ni Korea Kaskazini. Ni wazi magwiji wa teknolojia za silaha na vita wa magharibi watakuwa wanaumiza vichwa kumaliza undava ulioletwa nao wenyewe katika uvumbuzi wao wa silaha za nyuklia.