A
Anonymous
Guest
Taarifa kuhusu mchakato wa kufilisishwa kwa kampuni ya Sahara Media Group imeendelea kuvutia mjadala mpana hasa kwenye mitandao ya kijamii, huku wadau wengi wakibaki na maswali, pengine hata yasiyo na majibu ya moja kwa moja.
Kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea kufuatiliwa kwa kina, imeelezwa kuwa kampuni iliyotangazwa kufilisishwa ni Sahara Media Group, ambayo inadaiwa kwa sasa haina mali wala shughuli zinazoendelea. Wakati huo huo, inaelezwa kuwa vyombo vya habari vya RFA, Star TV na Kiss FM ni kampuni kamili zinazofanya kazi kwa utaratibu wao na hazihusiani moja kwa moja na kampuni iliyotajwa kufilisishwa.
Tukumbuke kuwa kumekuwapo na maswali mengi kuhusu hatma ya vyombo hivyo vya habari na iwapo vinaweza kutoweka sokoni kwa wakati mmoja.
Katika udadisi wa kutaka kujua mambo kwa kina, hoja nyingine inayojitokeza ni madai kuwa mchakato huo uliofanyika na uamuzi uliotolewa unaweza kuathiri moja kwa moja wafanyakazi pamoja na watu wengine ambao wamekuwa wakiidai kampuni hiyo kwa muda mrefu kutokana na kazi walizofanya. Baada ya uamuzi huo kutolewa, wingu la sintofahamu limezidi kutanda, huku maswali kuhusu haki na maslahi ya wadai yakizidi kuibuka.
Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, mtazamo unaojitokeza ni kuwa mbinu iliyotumika huenda ilikuwa na mpangilio uliosukwa kimkakati hadi kufikia hatua ya uamuzi uliotolewa kwa umma.
Pia soma ~ Kufilisika kwa Sahara Media: Kodi kubwa za TRA zinaua Biashara au ni Usimamizi Mbovu wa kina Diallo?
Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara, ndiyo iliyoamuru kufungwa kwa kampuni ya Sahara Media Group Limited, iliyojishughulisha na vyombo vya habari, matangazo na huduma za uchapishaji, kutokana na hali mbaya ya kifedha.
Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Dk. Mwajuma Kadilu baada ya kuridhia ombi la kufilisi lililowasilishwa na kampuni yenyewe. Ombi hilo liliungwa mkono na kiapo cha Afisa Mkuu wa kampuni, Steven Diallo, pamoja na nyaraka mbalimbali ikiwemo Memorandum and Articles of Association, azimio la Bodi ya Wakurugenzi, notisi za madai ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) – Mwanza, na taarifa za fedha zilizokaguliwa za miaka 2023 na 2024.
Katika uamuzi wake, Jaji Kadilu alisema kuwa ushahidi uliowasilishwa unaonyesha kuwa kampuni imepata hasara kubwa na haiwezi kulipa madeni yake:
“…ikiwa imethibitika kuwa mwombaji anapata hasara kubwa na hana uwezo wa kulipa madeni yake, basi hatua sahihi ni kufungwa kwa kampuni hiyo,” alisema Jaji Kadilu.
Kufuatia hali hii, maswali yanaibuka kuhusu uamuzi wa Mahakama na mkakati mzima unaodaiwa kusukwa.