Nyuma ya Pazia; TFF -AZAM TV Haki ya Matangazo

Okay, share hapa ilipotangazwa.
Hoja ya pili, contract duration na value for money unaizungumziaje, tunajadili Chief acha kupanic huenda ukajifunza kitu in the process
Hivyo ulivyotaja wewe vimefanyaje sasa? Usiwe pimbi ndio maana imeelezwa pesa itakuwa inaongezeka kwa kipindi chote cha miaka 10
 
Hizo gharama za uwekezaji zote ni sehemu ya consideration katika kutoa duration ya tenda, ndio unaona mikataba bandarini na sehemu nyengine ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa na maalum, ni nadra mzabuni kupewa tenda ya muda mfupi (kati ya mwaka mmoja na mi tano). Kwa vyovyote vile kama hakupata washindani waliopeleka andiko (proposal) bora kuliko zake (zote 2) haiwezi kuwa kosa lake, sababu huchagui washindani ktk mchakato wote wa tenda wala huwapangii washindani chakupropose.
Mara zote, ni vyema kuwa na taarifa zote kabla ya kutengeneza tuhuma, ni ajabu unatuhumu kuwa hakukuwa na tender iliyotangazwa, huwenda umeyasema bila kujua au ili kusajihisha malalamiko yako yaonekane yana mashiko, lakini hakuna wakati utangazaji wa tenda hizi umekuwa wazi kama sasa. Yashangaza kudai hakukutangazwa tenda hii!!
Kuwa miaka 10 ni mingi au si mingi, hili linaweza kuwa suala la mjadala, -mingi/si mingi ukilinganisha na nini ? Lakini suala kuwa mkataba huu utakwenda kupunguza changamoto za kiuendeshaji wa klabu sababu ya ukata, hilo ni wazi, si siri. Mkataba huu ukitekelezwa ipasavyo itasaidia klabu si changa tu, hata baadhi ya klabu kongwe kutatua changamoto nyingi za kifedha.
 
Neema imepatikana kuanzia TFF mpaka vilabu, funika kombe mwanaharamu apite, mambo mengine ni kuyaacha tu, kuna sheria, kanuni na taratibu nyingi kwenye mambo mengi tofauti tofauti zimevunjwa kwenye hii nchi, hili la TFF na Azam isiwe ajabu bana.
Wasiwasi yangu we shabiki wa simba bil20 aijatolewa lakini timu mshampa mmemwambia akalale nayo chini ya mto
 
Unaonaje wangepewa TBC? au basi Star TV?
 
Hivyo ulivyotaja wewe vimefanyaje sasa? Usiwe pimbi ndio maana imeelezwa pesa itakuwa inaongezeka kwa kipindi chote cha miaka 10

Nimefuatilia sana mada za MK54, kwanza jamaa nimuandishi mzuri sana namada zake huvutia kusoma.

kuna mambo mengi nilikuwa sijui na ninajiuliza lakini majibu nimepata kupitia uu uzi.lakini aliyekuwa na uthubutu wa kuuliza ni nani. Hivyo watu wanapoohoji tupunguze isia zetu na tuangalie hoja. Bongo tumepigwa sana na wawekezaji. Kupitia uzi hu tumejua kua tenda ilitangazwa, lakini ikumbukwe kwamba tenda nyingine hutangazwq kukamilisha taratibu za manunuzi tu lakini mambo yanakuwa tayari yameshasukwa.

Ninachoona hapa hoja ya msingi ya mleta mada ni hicho kifungo cha miaka 10. Kumbuka kila mwaka ubora wa ligi unaongezeka na kwa bongo mpira sasa ni dili ukizingatia tunatoa wachezaji kwenda kucheza soka la kulipwa nje. Je kulikuwa na haja gani ya kutoa mkataba wa miaka 10 badala ya miaka 5 au 4 huku tukiangalia ukuaji wa ligi yetu unamatumaini.

Pia ukisoma hilo tangazo lao, halioneshi kwamba mzabuni atakaeshinda atapewa Mkataba wa miaka 10, ni wazi kwamba hii ngoma imesukwa kwa ndani halafu nje ikaoneshwa kama pambo na kuna viashiria vingi vya asilimia kumi kuanzia ngazi ya juu. Hii ni wazi kabisa.sio kila kitu uje na rejea.hatupo kwenye uandishi wa ripot

Na wala usije kushangaa mkataba huu ukaja kuwa ni audit issue cag akifanya kazi yake . Sijui kama utarudi tena kwenye hu uzi.
Tuliaminishwa mikataba y ndege ilikuwa ni safi. Tumeona hoja za kikaguzi. Tuwe na akiba ya maneno kwenye haya mambo ya mikataba. Huwa nyuma kuna kuwa na ishu nyingi sana. Wasiwasi ndio akili yako na kuhoji ni ishara ya akili
 
Neema imepatikana kuanzia TFF mpaka vilabu, funika kombe mwanaharamu apite, mambo mengine ni kuyaacha tu, kuna sheria, kanuni na taratibu nyingi kwenye mambo mengi tofauti tofauti zimevunjwa kwenye hii nchi, hili la TFF na Azam isiwe ajabu bana.
...kuna sheria, kanuni na taratibu nyingi kwenye mambo mengi tofauti tofauti zimevunjwa kwenye hii nchi... POKEA KONGORE ZANGU.
 
Wewe ni tatizo. Una reasoning ya ajabu and very subjective. Na haujui lolote kuhusu manunuzi
We kichwa maji usiye jua hata Kama tenda ilitangazwa ni kupoteza Muda kukuelewesha.

Maana hujui tenda ilitangazwa lini halafu unabisha haijatangazwa ndiyo maana nimekuambia nenda kwenye page za Hamisa na juma lokole hao ndiyo wenzako.
 
Sina tatizo na udhamini lakini upande wa TFF hawakuwaza vizuri makubaliano ya miaka 10,ndani ya miaka 10 Azam wanaweza kufanya watakavyo maana hakutakuwa na mshindani mwingine,kutakuja mda hata vifurushi vya kuangalia mpira vitapandishwa na hamna uwezo wa kuhoji wakisema hawapati faida.

Imagine ndani ya miaka 10 ni derby ngapi za Simba vs Yanga itawaingizia hela nyingi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DStv wanadharau sana ligi yetu wacha waisome namba sisi na azam tu hata miaka 100
 
ukitaka kujua uwezo wa watanzania wengi kufikiri zije mada kama hizi watu wanaacha kujadili hoja wanamjadili mtu binafsi.
Hoja hujibiwa kwa hoja.
 
Hoja hiyo ya vifurushi kupanda ni dhahiri. kwa mpunga uliowekwa usitegemee bando likawa 20k kama ilivyo sasa. Azam hawafanyi charity pale wanafanya biashara. Tegemea hilo.
Kama hutaki kulipia nenda viwanjani kaangalie mbona simpo tu. Kama dstv wanatoza 80k kuangalia EPL kwaniAzam.walitoze 40k kuangalia ligi.


Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
Tumejaaliwa wajinga kwenye hili taifa, hadi raha
 
Okay, share hapa ilipotangazwa.
Hoja ya pili, contract duration na value for money unaizungumziaje, tunajadili Chief acha kupanic huenda ukajifunza kitu in the process
😂 Hebu ficha upumbavu kwa kukaa kimya

Tenda ilitangazwa kwenye vyombo vyote vya habari hata humu jamii forum ipo wadau walileta

Hakuna kampuni yeyote ingeweza toa bil 220 zaid ya azam , kimsingi hakuna ambae angevuka hata bil 5 kwa mwaka

DStv atoe hiyo pesa kwa miundo mbinu gani aliyonayo hapa nchini? Watanzania wanaofuatilia Ligi ya Tanzania n wangapi wanaweza lipia DSTV?? Kwamba DSTV wao n wapuuz wamwage tu pesa ambazo wanajua hawatoweza rudisha? Hebu acha ujinga

Unafananisha ligi ya bongo vs South Africa?
 
Kwamba hutaki Azam wapige pesa? Hizi akili za kimasikini baadhi yenu zipo damuni kabisa
 

Mkuu karibu sana katika majadiliano ya HOJA. Ninaamini unajua sheria za manunuzi kwa namna moja.
-
Kutangazwa kwa tenda haimaanishi chochote kama mchakato mzima wa manunuzi ukiwa COOKED. Kutangaza huko inakuwa ni kukamilisha taratibu ili ionekane taratibu zilifuatwa.
-
Kama ulivyosema HAKUNA kampuni yoyote ambayo ingezeweza , hayo ni majibu yako kabla ya mtihani.
-
Wewe umeona TANGAZO , sisi tumeeona Tender Document ambayo kimsingi Bidders were not informed in advance kuwa the contract duration itakuwa ni miaka 10 . Hata ukiangalia hako katangazo kako ka invitation to tenderers unapata majibu.
-
Kwa mujibu wa PPA’11, Framework Agreement ni miaka 2. Lengo kuu ni to take into consideration value for money and price fluctuation over time as well as demand variations. Kwa mfano kuna uwezekano ndani ya miaka 2 ijayo, active customers wa AZAM ambao ni registered waka double au increase significantly, while PIN ya AZAM itakuwa pale pale ni bil 225 kwa miaka 10 ; wakati huo huo kuna demand increases , price fluctuation kwa maana baada ya demand ikiongezeka, kuna uwezekano price ya kuona hayo matangazo ika shoutout, kwa sababu tayari Mkataba ulishasainiwa, there is no room wewe to amend contract terms .

I am pretty sure utakuja kulia lia hapa hapa JF. Hii ndiyo sababu tunahoji contract duration ya huo mkataba on which GROUND ? Kufanya hivyo ni kufunga milango ya kuboresha mapungufu SUPPLIER yaani Supplier Performance.

Aidha, ukifanya Performance Evaluation ya existing Contract, hajafika 55% . Kuna watu wengi walikuwa wanashindwa ku access hizo matches na channels despite kwamba mtu kalipia. Kuna mechi nyingi zilikuwa za KUMRADHI hatutoweza kuonesha match fulani kwa sababu fulani.....hiyo ndiyo maana ya Supplier Performance na inatoa ROOM kumpin service provider wakati wa contract renewal. Sasa umempa miaka 10 ya UHAKIKA, kwa Sheria za manunuzi maana yake ni HARUFU , and it has to be investigated.

Ni sawa na ule MKATABA wa Bagamoyo, ni PIN ya muda mrefu, MWENDAZAKE akausimamisha kwa sababu ulikuwa ni ANGAMIZO japo kwa nje ulionekana UNATIJA.
-
Tunapojadili haya mambo wengi huonesha HISIA badala ya UHALISIA ; hii ndiyo shida ya KIZAZI hiki, uwezo wa kufikiri upo chini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…