SI KWELI Nyumba 480 kata ya Mikocheni zimeingiziwa mfumo wa gesi

SI KWELI Nyumba 480 kata ya Mikocheni zimeingiziwa mfumo wa gesi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima amesema mojawapo ya sehemu zinazopatikana kwenye Jimbo lake inayoitwa Mikocheni wamefanikiwa kusambaza mabomba ya gesi kwenye nyumba 480.

Uhalisia wa kauli hii upoje wakuu?


images.jpeg

Picha: Sample​
 
Tunachokijua
"Kule kwenye Jimbo la kawe tumefanya hii study, tumeamua kuingiza gesi kwenye nyumba 480, wamewekewa gesi, wana mita. Mwenge wa uhuru ulipita pale, kwenye kila nyumba, kwenye nyumba 480 na kitu. Yule mtu alikuwa anatumia umeme wa Tsh. 50,000 sasa hivi analipa Tsh. 5,000 hadi 10,000."

Haya ni maneno yanayosikika yakizungumzwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe (CCM) Josephat Gwajima akiwa Bungeni wakati anachangia hoja kwenye mjadala wa mpango wa Taifa wa mwaka mmoja (2025/26). Mchango huu aliuchapisha pia yeye mwenyewe kwenye ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa Instagram Novemba 8, 2024. (Hapa)

Kwa mujibu wa Sensa ya Mwaka 2022 iliyochapishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Jimbo la Kawe lina jumla ya wakazi 648,744 huku Kata ya Mikocheni iliyotajwa na Gwajima ikiwa na wakazi 25,433 wanaoishi kwenye kaya 7325. Hii inamaanisha kuwa, 6.6% ya nyumba za wakazi wa kata hii wamewekewa gesi majumbani.

Ikumbukwe kuwa, Aprili 4, 2024, Gwajima aliuliza swali Bungeni ni lini Serikali itaweka mabomba ya gesi Jijini Dar es Salaam kila nyumba, ili wananchi wapikie nishati hiyo nafuu ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alibainisha kuwa tayari Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lilikuwa limesambaza gesi asilia kwa njia ya mabomba katika nyumba 880 katika Jiji la Dar es Salaam huku Mikocheni ikiwa na nyuma 155 pekee. Unaweza kutibitisha hapa.

Kapinga aliendelea kueleza kuwa Serikali imejenga bomba la gesi lenye urefu wa kilomita 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach kupitia barabara ya Bagamoyo, bomba lenye matoleo katika maeneo mbalimbali, ili kuweza kuunganisha wateja wa majumbani.

Takwimu za sasa zinasemaje?
JamiiCheck imefuatilia madai haya ya Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima na kubaini hayana Ukweli.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi ambazo JamiiCheck imezipata kutoka TPDC, leo Novemba 14, 2024, Kata ya Mikocheni ina nyumba 210 pekee zilizowekewa mfumo wa gesi ambapo Mikocheni TPDC - 70 na Mikocheni, Mlalakua - 140. Aidha, sehemu zingine za Jiji la Dar es Salaam ambazo ni Sinza, Kurasini na UDSM zina nyumba - 226, 344 na 100 mtawalia.
Ameshindwa kujengaa vyoo tu pale stand ya Kawe ataweza la mabombaa....??

Mazingira ya stend ya Kawe ni machafu na hatarishi sana.
 
Kinachosikitisha Zaidi huyu ni kiongozi wa dini na kuna watu wanamuamini kabisa na kila siku wanaenda kanisani kwake kupata mafundisho. Aisee kama mbingu ipo, wachache sana wataiona.
 
Ahadi za gwajima za kampeni ngapi zishatimia? Alitaka kupeleka watu "bamingam"
 
Back
Top Bottom