Nyumba, Duka vinauzwa na NMB Bank

Bora mtu mwenyewe auze ili kulipa mkopo ila sio kufukuzwa na bank then waiuze ni hatari usijaribu ,900 itapendeza.
Hivi benki hawaweki option ya mwenye nyumba kutafuta mteja na akipata auze chini ya usimamizi wa benki? Nchi nyingine ukinunua nyumba kwa mkopo na ukashindwa kumaliza deni katikati, unaruhusiwa kumpa agent atafute mteja wa kununua hiyo nyumba na akipatikana benki inachukuwa inachodai na kama fedha zimebaki zinakuwa za mteja.
 
Cc: Mshana jr
 
Usithubutu kununua!! Utarogwa kuna jamaa yangu yupo mikoa ya kusini, alijaribu kununua nyumba ya namna hiyo, bado kdg roho ichomoke, watu wakamstua kuwa huku wazee wakikopa, na benki wakatangaza mnada, huwa hawajitokezi maana mwenye mali anaweka uchawi kwenye hizo mali, ye alikuwa mgeni na hela zake uhamisho hajui hili na lile, akaenda kwenye mnada, almanusura roho ichomoke na bahati yake alipozinduka hospital, yule mzee alimuibukia akamwambia pole sana kumbe we u mgeni? Basi utapona ukaendelee na maisha yako, ila usikurupuke kununua vitu vya madeni na madai
 
Huu ni uongo. SIyo kweli. Kwani mnunuzi ana kosa gani? Nawajua watu wengi tu walionunua nyumba za aina hiyo na wanaishi vizuri kabisa. Hii imani ya kijinga kabisa imebuniwa na wadaiwa sugu ili kuwatisha wanunuzi wa nyumba za aina hii.
Ni kweli mkuu, hata mimi nilikuwa najifanya msomi saana, kila aliyekuwa ananiambia habari kama hizi nilimuona mjinga na punguani, hata habari za mila nilikuwa naona ni ujinga mtupu mkuu.

Ukisema watu wengi nakuelewa kabisa, kila nyumba inayouzwa iliyokopewa ina simulizi yake na hali yake ya kipekee. Nakiri pia sio zote. Wengine huwa wanakopa na hawalipi makusudi ili nyumba iuzwe, na wengine ni waelewa, wanajua madhara ya kutokulipa deni.
 
Big big NO. Hii ni imani ya upuuzi kama imani nyingine.
 

Nyumba zinazouzwa baada ya mtu kushindwa kulipa mkopo hapana kwakweli! Unakaa ndani usiku upo na mkeo, unasikia mtoto anacheka bafuni na wakati hamna mtoto.

Upo ndani peke yako ila unahisi umepishana na mtu kabisa wakati unaenda chumbani.
Acha utoto basi!
 
Huu ni uongo. SIyo kweli. Kwani mnunuzi ana kosa gani? Nawajua watu wengi tu walionunua nyumba za aina hiyo na wanaishi vizuri kabisa. Hii imani ya kijinga kabisa imebuniwa na wadaiwa sugu ili kuwatisha wanunuzi wa nyumba za aina hii.
Lakini Mkuu kumbuka kuna nyumba mtu anakopea Bank kwa makusudi kabisa akiwa kadhamiria kutolipa mkopo huo.Mara nyingi unakuta thamani ya nyumba ilikuwa inflated kuliko uhalisia na mtu anachukua mkopo mkubwa kuliko thamani ya nyumba.Hizo ukiuziwa hazina shida.

Kuna hizi ambazo waliokopa walikuwa na nia ya dhati ya kulipa lakini wakashindwa na nyumba ikauzwa huku wanalia machozi.Hizi ni za kuogopa sana kuzinunua.
 

Raha ya humu mitandaoni si hatujuani mkuu, huwa tunajifanya hatuna imani kabisa na mambo ya mazingaombwe, hatuamini uchawi. Ogopa sana unanunua nyumba kwenye mnada na mwenye nyumba yake yupo hapo machozi yanamtoka.

Kwa mliopo mjini Dar, kuna nyumba kadhaa tu zimetelekezwa, watu hawakai!
 
Daaah Ngujini, Kirongwe, Kirongaya, Ndanda to Lomwe, Baghdad mitaa flani bandidu sana
 
Za kuogopa vipi? Hujui dawa ya deni ni kulipa? Akilia machozi hiyo ni shauri yake kwani alipokuwa anakopa alikuwa anajua yote haya. Yaani unataka kunidanganya kuwa kwa mfano mimi nikija kwako kukukopa sh. milioni 50 nikajengea nyumba halafu nikashindwa kulipa, ukichukuwa ile nyumba, mimi nikilia basi ile nyumba italaanika?
 
Nasikia jamaa alimpigaga tukio bosi wake wazamani ndio akapata mtaji wakuanzisha duka lake, itakua laana ya bwana gopali.
Hii issue niliisikia leo mtaani,Gopali akaacha laana flani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…