Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri bin Salim al Harith

Mwaka 1914 ulikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, na si ya Pili kama ulivyoandika. Pia nashauri uwe unaandika ulivyovipata, kisha maoni yako yawe mwishoni.
 
Mji wa Pangani umetekelezwa..uchumi wake haukui. Umedumaa mno.Majengo yake bado ni ya kizamani.
majengo hayo huingiza pesa za kigen nying kupitia utalii kwa kuyaweka katika hali nzuri
 
Mwaka 1914 ulikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, na si ya Pili kama ulivyoandika. Pia nashauri uwe unaandika ulivyovipata, kisha maoni yako yawe mwishoni.
James,
Ahsante sana nimekosea tarehe nitasahihisha.

Kuhusu maoni.

Hupenda kuunganisha hapo kwa hapo ili nisimwache nyuma msomaji.
 
Maandiko yako ni elimishi lakini mara zote huwa yana mlengo wa kidini! Siku zote unaandika kwa namna ya kulalamika.
Trace...
Umesema kweli kabisa.

Wakoloni waliwachukua Waislam kama maadui zao na wakafanya kila hila kuwahujumu.

Hii ndiyo sababu Wajerumani katika Vita Vya Maji Maji waliwanyonga makamanda zaidi ya 60.

Makaburi yao yapo Mahenge, Songea.

Walipokuja Waingereza hali haikubadilika na Waislam wakaunda African Association kuwakusanya Waafrika kwenye umoja ulikuja kuzaa TANU.

Historia hii ilipokuja kuandikwa ilifanyiwa hujuma kubwa.

Nimenyanyua kalamu kusahihisha historia hii kwa kueleza nafasi ya Uislam na Waislam katika kupambana na ukoloni.
 
Maandiko yako ni elimishi lakini mara zote huwa yana mlengo wa kidini! Siku zote unaandika kwa namna ya kulalamika.
😍😍😍😍😍😍😍😍 Nami huwa namuona hivyo. Mohamed ni mwandishi anayependa udini na kuutelekeza utaifa.
 
Japo huwa napingana na mlengo wako, hakuna shaka. Abushiri alikuwa shujaa na bado ni shujaa wetu. Historia mara nyingi, kama alivyowahi kusema Winston Churchill, huandikwa na washindi. Hivyo, hupotosha mambo mengi ya msingi. Adui yako anapoandika historia yako, lazima atakudhoofisha na kukusingizia. Hii ndiyo maana historia hufanyiwa marejeo, marekebisho hata kuandikwa upya inapobidi.RIP SHUJAA ABUSHIRI BIN SALUM
 
Mzee Mohamad Said, asante kwa taarifa yako. Nimesoma sasa hivi taarifa tofauti. Kuna kitabu cha Kijerumani kilichoandikwa na H.F. von Behr, luteni katika kikosi cha Wissmann kilichokandamiza upinzani wa watu wa pwani manmo 1888/1889. Kitabu ni "Kriegsbilder aus dem Araberaufstand in Deutsch-Ostafrika, Leipzig 1891", pamoja utangulizi uliotungwa na Wissmann. (yaani "Kumbukumbu ya vita wakati wa uasi wa Waarabu katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)
Kinapatikana kupitia google-books.
Mlango wa 15 na wa mwisho unaitwa "Kukamatwa na kifo cha Bushiri". (uk. 329-336)
Kufuatana na taarifa hiyo, kwenye Disemba 1889 kombania mbili za askari chini ya kapteni Schmidt kilimfuata Abushiri hadi "Muenda" kwenye eneo la "Nguru" (yaani Ungulu) . Hapa walishambulia kambi la Abushiri aliyeweza kukimbia. Tarehe 7 Disemba Schmidt alipata ujumbe kutoka jumbe Magaya kuwa Bushiri alikamatwa mahali panapoitwa "Quamkoro" ; kufuatana na taarifa ya Behr maili 20 za Kijerumani, yaani kilomita 140 kutoka "Muenda".
(Kwenye ramani ya google naona eneo la msitu wa Kwamkoro, kati ya Muheza na Korogwe; "Muenda" sijakuta; "majumbe" walikuwa ama machifu wadogo au viongozi ya eneo dogo waliopewa nafasi yao na Sultani )

Walimkuta Abushiri katika nyumba moja alipofungwa. Behr alieleza alikuwa nusu-uchi, akivaa kikoi pekee, mikono na miguu ikifungwa kwa nyoro za chuma; kichwa kilifungwa katzika uma ya mti jinsi ilivyokuwa kawaida kwa watumwa waliosafirishwa. Walimpeleka Pangani wakimweka juu ya punda (Behr aliandika Abushiri alikuwa na miguu iliyovimba ).
Behr anasimulia jinsi Abushiri alihojiwa na Wissmann aliyefika na jinsi alivyonyongwa mnamo saa 10 tarehe 15 Disemba. Baada ya kifo walifika ndugu zake wakapewa mwili wakazika usiku uleule.
Naongeza picha iliyopo baada ya ukurasa 331. Maelezo yake ni "Buschiri's Gefangennahma" (Kukamatwa kwa Abushiri). Kitabu hakina maelezo picha zilichorwa na nani; kama ni kweli, walimpa blanketi avae baada ya kumtoa kutoka kitanda alipofungwa, akisimama pamoja na afande na askari Wanubi.
 
Mwana...
Nakushukuru sana kwa taarifa hii yako.
Kuna baadhi nilikuwa nimeyasikia lakini yamepotoshwa kidogo.

Kukamatwa kwake nimesoma ni kuwa alisalitiwa na jamaa mmoja kabila Mzigua.

Wakati huo Bushiri aliwekewa dau la rupia nyingi kwa mtu atakaemkamata.

Bushiri taarifa hiyo alikuwa yuko njiani akijaribu kukimbilia Mombasa.

Iko picha ninayo mahali ya Bushiri kavaa blanketing.

Ahsante sana.
 
Huyu Magaya aliyemkamata kuwa Mzigua nimesoma kwa Iliffe, Modern History of Tanganyika, uk.96f.
Ile uliyoandika juu kuwa Wajerumani walitaka kuficha kaburi lake sijaona uthibitisho; kufuatana na Behr ndugu zake walimzika.
Behr mwenyewe katiba kitabu chake anampa heshima kiasi akisifu uwezo wake kama kiongozi wa pekee aliyewapa Wajerumani matatizo makubwa.
Binafsi sijaelewa bado kwa nini walitaka kumnyonga wakati walimsamehe Bwana Heri bin Juma kiongozi wa Saadani. Labda kwa sababu walipaswa kufuata propaganda yao (maana walipata kibali cha bunge la Ujerumani tu kwa kudai, eti hapa ni vita ya kupambana na Waarabu wafanyabiashara wa watumwa) ? Au kwa sababu Wissmann alikumbuka msaada wa Bwana Heri aliopata miaka ya nyuma? Au kwa sababu hakumwona Bwana Heri kama "Mwarabu"? Labda kwa sababu Abushiri hakuwa tena na wafuasi wengi lakini Bwana Heri alikuwa na kundi kubwa hivyo waliona afadhali wapatane naye?(ona zaidi hapa Bwana Heri - Wikipedia, kamusi elezo huru)
 
Nimenyanyua kalamu kusahihisha historia hii kwa kueleza nafasi ya Uislam na Waislam katika kupambana na ukoloni.
Kwani mkuu kuna hujuma zozote zinafanywa kuonesha kua waislamu hawakupambania uhuru??

Mimi naona hostoria zinaelezea utaifa zaidi na sio udini zaidi, mfano hao wapigania uhuru na kama hao kina bushir, mkwawa wanatajwa tu majina yao na sio dini zao labda tu watatajwa kanda wanazotoka.

Imekuaje unalalama hivi kuhusu hiyo diji mkuu, kuna namna yoyote mnahujumiwa kwenye historia??
Au unataka dini ipewe heshima na isomwe mashuleni kua ni dini iliyoahiriki kupigania uhuru, naomba nieleweleshe hapo ndgu.
 
Maandiko yako ni elimishi lakini mara zote huwa yana mlengo wa kidini! Siku zote unaandika kwa namna ya kulalamika.
Kweli hii ni changamoto kubwa kwa Mzee wetu halafu ulalamishi wenyewe mm sioni mantiki maana Wote Abushiri tumemsoma mashuleni ila hapa Mzee anakwambia majina yao yamekwepwa ila kwa upande wangu leo ndio nimesikia kuwa kumbe Mutwa Mukwava mukwavinyika Akiitwa Abdalah kiukweli nilikua sijapata kulisikia jina hili kabla
 
😍😍😍😍😍😍😍😍 Nami huwa namuona hivyo. Mohamed ni mwandishi anayependa udini na kuutelekeza utaifa.
Ulitaka asiipende dini? Wewe huna dini?
Mji wa Pangani umetekelezwa..uchumi wake haukui. Umedumaa mno.Majengo yake bado ni ya kizamani.
darcity nadhani ulitaka kuandika "umetelekezwa".

Kuhusu majengo ya kizamani, ni vyema wakayaacha lakini wawe wanayakarabati, ndio historia yenyewe hiyo.

Naona wenyewe wanyeji wa Pangani wamezubaa, mashamba ya nazi wanayauza badala ya kuuza nazi, na fukwe zao zote wanauwauzia wageni. Pesa wanaolea wake na kulia pilau.


Mwisho itakuwa kama Unguja, mpaka sasa nadhani 80% ya fukwe zake inamilikiwa na Wataliano,(nahi ni Vatikano au mawakala wake). Kama si wao vile, wanashambulia kimkakati.

Si Pangani tu, tufunge vibwebwe, pwani yote ya Afrika Mashariki, kwenye chimbuko la Uislam, tunaipoteza kwa Wataliano, kidogo kidogo. Historia njema ya Waislam inafutwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…