Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri bin Salim al Harith

Ni kweli nilimaanisha hivyo...nashukuru na nimefurahi kuona mchango wako Jamii Forum ingawa umeadimika.

Nilikuwa huko kikazi miaka kadhaa nyuma. Unachosema ni kweli fukwe nyingi zimeuzwa na zao la nazi linaporomoka wakati mahitaji ni
mengi.
 
Kwanini msiwashawishi waarabu muwauzie fukwe hizo

Ova
 
Kwanini msiwashawishi waarabu muwauzie fukwe hizo

Ova
Mwarabu gani wa kununua huko?walichokipata mapinduzi 64 kinawatosha.hao koko waliobaki ni masalia tu ya wale waliokimbia.
 
Bushiri alikuwa mwarabu wa Oman?
 
Kwa hiyo most probably alikuwa anapigania inerest zilizomleta, na tunajua ni interest gani.
Lole...
Huna sababu ya kudhani.

Ingia Google kaandikwa na wasomi wengi Abushiri pamoja na Wajerumani wenyewe.

Abushiri kwao Zanzibar alihama akaja Pangani kwa kuwa Wajerumani walimdhulumu mali zake.

Nenda leo Zanzibar Mambo Msiige ukatazame mali zake.

Pangani akatajirika lakini aliona dhulma za Wajerumani pale na pwani yote ndipo alipoamua kuwanyanyulia silaha.

Huna la kusema kuhusu interest za Wajerumani na Leipzig Mission?
 
Mzee samahani kwa kawaida una elimu nzuri ya historia lakini hapo uko mbali kidogo. Abushiri alipoondoka Zanzibar mnamo mwaka 1870, Wajerumani hawakuwepo pale na mamlaka yoyote. Walifika Zanzibar wakati ule kama wafanyabiashara pekee wasio na madaraka. Abushiri hakuelewana na akina Sultani akaeleza mwenyewe kwamba hakumtambua tena Sultani kama mtawala anayestahili kuwepo.
Halafu nashangaa unataja Leipzig Mission??? Hao hawakufika Tanzania hadi 1893, wakati Abushiri alikuwa ameaga Dunia tayari.
 

Bwana Heri Ibn Juma alikuwa sultan wa Saadan wakati Abushir akiwa mfanyabiqshara wa Pangani. Hapa chini
katikati huyo ni Bwana Heri
 
Mwana...
Tunazungumza kuhusu, ''interests,'' za Abushiri.

Katika kutafuta maslahi yake ndipo nikaeleza kuwa Abushiri alikuwa Mzanzibari baba Mwarabu mama Mwafrika.

Zanzibar ni kwao sasa mtu kumuuliza Mwafrika tena mtu wa pwani kafata nini Pangani na Bagamoyo kidogo nimeshangaa ndiyo nikauliza mbona Leipzig Mission walifika na tukawapokea?

Hutushangazwi na hawa?
 
Andiko lingine bora kutoka kwako


Hii tabia ya kuwaita mashujaa wetu waliojitolea uhai wao kwa uhuru wetu kuwa ni waasi ni tabia dhalili sana.

Mzee Mohammed narudia tena na tena, weka haya maandiko kwenye mfumo wa vitabu.

Kuna mengi yanayoumiza masikio na hasa sisi wengine tusiyopenda kuyasikia yanahitajika kusemwa. Historia kama ya Abushiri na Bwana Heri hazikuwekwa bayana ya kuwajuza wajukuu nini kilitokea. Kwa mfano tunasoma kuhusu Tipu Tip kama mtu mashuhuri sana wakati ndiye aliyekuwa dalali biashara ya Watumwa.

Tujue kwa vipi na namna gani Sultan Bharagash aliweza kuitawala Zanzibar na Pwani. Hakuna maandishi zaidi ya namna wazungu walivyoingia Nchini mwetu
 
Abdallah...
Umesema kweli kabisa.

Naandika historia iliyochukiwa na wakoloni wakaifanyia khiyana.

Kama nisingeandika historia hii wewe ungeijuaje?
Kwenye hili nakuunga mkono ingawa nitakupinga kwa hoja kulingana na mtazamo na ufahamu wangu
 
Huyo Abushiri ana asili ya nchi gani?
 
Yani hadi machozi yanataka kunitoka. Kiasigani wakoloni walituweza.

Hongera sana kwa kutuelimisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…