Nyumba inanuka udi, ukaguzi ukafanyika, vipande vilikutwa kwenye pochi ya mke wake

Nyumba inanuka udi, ukaguzi ukafanyika, vipande vilikutwa kwenye pochi ya mke wake

Benno

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2009
Posts
332
Reaction score
51
"katika ugomvi wa mke na mume, mke aliamua kwenda kutafuta udi na kufukiza chumbani na mwilini mwake"

mume aliporudi na kupata mshituko wa harufu iliyotanda ndani, mke alidanganya kuwa ni harufu ya net kwa sababu ni mpya,
baada ya mume kupekua alikuta vipande vya udi ndani ya mkoba wa mke wake.

Baada ya kuhoji sana mke aliishia kulia mpaka sasa haijulikani ni nini kilifanyika.

'nimeamua kulala nje ya nyumba, hadi nitakapopata ufumbuzi"

wadAU mnisaidie
 
Kwani udi una matatizo gani ?nijuzeni kwani mie sio mtumiaji ila nasikia wadada hujifukiza wanukie vizuri Una kazi nyingine???????///
 
rudi nyumbani,udi hauna lolote.wengi huwa wanaamini hutumika katika ushirikina lakini kwa imani yangu hakuna lolote.mpige tu biti hupendi hiyo harufu na kama anaimani hizo akome.
 
Wadau, Huo udi umetoa tuu HArufu ila Nahisi kutakuwa na mchanganyiko wa Madawa Mbalimbali, Kwani wengine wanasema UDI ni chakula cha Mashetani sasa kwa mimi ,,,,,,,,,,,,,,,,,

Kazi ipo
 
Udi kwani si ni sawa na perfume nyengine tu?

Tofauti yake huwa harufu inabaki kwa muda mrefu hata mwilini au kwenye nyewe

Sijaona tatizo hata dogo
 
teh teh sio kila tunaloambiwa kwenye kitchen party tunalibeba kama lilivyo....mengine unaweza shtukia talaka hivi hivi,mwambie huyo kaka amsamehe..was honest mistake na pia anahitaji kuelimishwa udi hauhusiani na madawa ya kishetani ni perfume tu...aache kuchachawa.:whoo:
 
Subhana llaaah!!!!! Jamani nini teeena???ni huu udy niujuao. Au ni kipi?
 
udi wa mapenzi au ule wa ibada?maana kuna udi hutumiwa na katoliki au waislam!Alimkuta kavaa kanga moja?kama ni wa kina mama Mimi ningekuta hivyo moja kwa moja kitandani,harufu ya udi huamsha hisia za mapenzi!wanawake wa tanga anaweka na hiliki kwenye maji ya kuoga!
 
Udi kwani si ni sawa na perfume nyengine tu?

Tofauti yake huwa harufu inabaki kwa muda mrefu hata mwilini au kwenye nyewe

Sijaona tatizo hata dogo

gaijin, kunukia tu? Mh hadi kwenye pochi?
 
tooba , yaani ndiyo kwanza umentia hamu hapa nimechutamia chetezo uturi nimeutia wa kutoshea yaani chumba kizima kinanukia utamu , unakosea kuuita udi unaitwa uturi
 
Udi gani unazungumzia? Kama ni udi wa uturi ni wa kumfanya mwanamke na mazingira yake ya chumbani kuwa na harufu ya kunukia vizuri na kupendezesha. Hauna uchawi wo wote.

Ule udi mwengine ndiyo ukichonmwa unaainisha labda maombi fulani lakini sioni uhusiano nao.
 
Bro umenikumbusha mshkaji wetu mmoja(RIP) demu wake nae alijifukiza hayo makitu "kunako" wakati wamemaliza majambozi anashangaa mzee wake kajaa masizi na mavitu meusi meusi yananukia udi... kumbana demu akakiri kuwa aliambiwa na rafiki yake hiyo kitu inazidisha raha akaamua kutest zali. Alimpiga marufuku demu akaachana na hayo makitu...

Usiwe na wasi wasi ni mambo ya kawaida mademu wanafundishana tuu...
 
Bro umenikumbusha mshkaji wetu mmoja(RIP) demu wake nae alijifukiza hayo makitu "kunako" wakati wamemaliza majambozi anashangaa mzee wake kajaa masizi na mavitu meusi meusi yananukia udi... kumbana demu akakiri kuwa aliambiwa na rafiki yake hiyo kitu inazidisha raha akaamua kutest zali. Alimpiga marufuku demu akaachana na hayo makitu...QUOTE]

Huyo hakuhitimu mafunzo alikurupuka tu. Kwanza siku hizi kuna vyetezo (vile vya kufukizia) vya umeme, na vyengine vya makaa ya mawe kwa hivyo hiyo kitu masizi ni historia. Na vile vile kitamaduni kuna 'stand' yake ya kufukizia kwa hivyo nguo na mwili huwa havigusi huo mkaa.
 
Udi kwani si ni sawa na perfume nyengine tu?

Tofauti yake huwa harufu inabaki kwa muda mrefu hata mwilini au kwenye nyewe

Sijaona tatizo hata dogo

Kwa kuongezea ... ni tofauti za tamaduni tu. Perfume za kimagharibi, udi ni watu wa mwambao na bara Arab. Kazi yake ni ile ile kutia harufu nzuri na kuondoa harufu zisizohitajika.Ndio maana hufukizwa kwenye nguo, mwili pamoja na nywele, matandiko, mapazia na hata chumbani.
Huyu ndugu inaelekea ni mgeni wa mambo haya na huyo mkewe huenda ndo kwaanza katoka kupewa somo na mashosti na somo bado halijakolea sawasawa, anashindwa hata kumwelewesha mumewe kikaeleweka.

Kukuta vipande kwenye pochi si ndio udi wenyewe? Udi waweza kuwa wa namna/aina nyingi kutegemeana na ulivyopikwa.Waweza kuwa kama hivyo, au kuwa na chengachenga maana wakati mwingine hupikwa na sukari nk.
 
Bro umenikumbusha mshkaji wetu mmoja(RIP) demu wake nae alijifukiza hayo makitu "kunako" wakati wamemaliza majambozi anashangaa mzee wake kajaa masizi na mavitu meusi meusi yananukia udi... kumbana demu akakiri kuwa aliambiwa na rafiki yake hiyo kitu inazidisha raha akaamua kutest zali. Alimpiga marufuku demu akaachana na hayo makitu...QUOTE]

Huyo hakuhitimu mafunzo alikurupuka tu. Kwanza siku hizi kuna vyetezo (vile vya kufukizia) vya umeme, na vyengine vya makaa ya mawe kwa hivyo hiyo kitu masizi ni historia. Na vile vile kitamaduni kuna 'stand' yake ya kufukizia kwa hivyo nguo na mwili huwa havigusi huo mkaa.
kuuliza si ujinga...nijuavyo mimi udi ni kama air freshner na perfume..but yatumika tena mtu akitaka kulala ?!!
 
Kwa kuongezea ... ni tofauti za tamaduni tu. Perfume za kimagharibi, udi ni watu wa mwambao na bara Arab. Kazi yake ni ile ile kutia harufu nzuri na kuondoa harufu zisizohitajika.Ndio maana hufukizwa kwenye nguo, mwili pamoja na nywele, matandiko, mapazia na hata chumbani.
Huyu ndugu inaelekea ni mgeni wa mambo haya na huyo mkewe huenda ndo kwaanza katoka kupewa somo na mashosti na somo bado halijakolea sawasawa, anashindwa hata kumwelewesha mumewe kikaeleweka.

Kukuta vipande kwenye pochi si ndio udi wenyewe? Udi waweza kuwa wa namna/aina nyingi kutegemeana na ulivyopikwa.Waweza kuwa kama hivyo, au kuwa na chengachenga maana wakati mwingine hupikwa na sukari nk.

Mama weye mtaaluma kwer kwer.
 
Back
Top Bottom