nazani hivi ndivyo alivyokusudia muanzisha sredi, hawa walioleta habbar za shetani na iblis nazani wanamiss point.kuna kitu hamjaelewa hapa. huyu mama alikuwa anajiandaa kwenda kujirusha na kidume kinachopenda uudi na mzee akamkwida aeleze nani kamuagiza ajifukize manake mzee wake hana mazoea wala interst na uudi. kwa kweli huyo mwanamke anatakiwa kibano cha nguvu hadi ataje hilo buzi lake la kimwambao na kisha kisago na baadaye talwaka 30! nyambaf!
nazani hivi ndivyo alivyokusudia muanzisha sredi, hawa walioleta habbar za shetani na iblis nazani wanamiss point.
Mi nadhani unyumba anaupata kwa mbinde. Jibaba lipo lipo tu ka zigo. Katika kujitahidi afanyeje kumvutia mumewe kimapenzi, ndo kashauriwa ajifukize udi, baba akirudi akisikia harufu hiyo nzuri mambo yatakuwa shwari. Kumbe jibaba hilo nalo, ndo limezidisha vituko, limelala nje kabisaaaaa! Kazi anayo huyo mwanamke mwenzangu. Nyie wababa mwelimisheni mwenzenu. Hapo tatizo liko kwenye unyumba mama anahaha tu kutafuta namna ya kumfanya baba achangamkie. Bibie akikaa ka zigo anaambiwa mshamba, akianza kutafuta utaalam anakimbiwa alale mwenyewe. MWE! :humble:
Kwa kuongezea ... ni tofauti za tamaduni tu. Perfume za kimagharibi, udi ni watu wa mwambao na bara Arab. Kazi yake ni ile ile kutia harufu nzuri na kuondoa harufu zisizohitajika.Ndio maana hufukizwa kwenye nguo, mwili pamoja na nywele, matandiko, mapazia na hata chumbani.
Huyu ndugu inaelekea ni mgeni wa mambo haya na huyo mkewe huenda ndo kwaanza katoka kupewa somo na mashosti na somo bado halijakolea sawasawa, anashindwa hata kumwelewesha mumewe kikaeleweka.
Kukuta vipande kwenye pochi si ndio udi wenyewe? Udi waweza kuwa wa namna/aina nyingi kutegemeana na ulivyopikwa.Waweza kuwa kama hivyo, au kuwa na chengachenga maana wakati mwingine hupikwa na sukari nk.
kuuliza si ujinga...nijuavyo mimi udi ni kama air freshner na perfume..but yatumika tena mtu akitaka kulala ?!!
demu alijiwekea ukeni hayo makitu ya kunukia ili kumvutia jamaa... si kwamba ni kwa ajili ya kulala. Na alibanwa akasema alielekezwa na rafiki zake jinsi ya kupagawisha.