Ina vyumba vitatu. Ipo kijitonyama Kisiwani. Ipo vizuri sana. Inapangishwa kwa sh 400,000 kwa mwezi. Maelewano yapo. Wahi usichelewe. Mawasiliano 0784 225 000
Kitu kimesimama hiki kwa wale wenye nyumba ndogo changamkeni
nzuri sana tatizo ka TGS D kote kataishia humo kwenye kodi
Mbona cm yako tunakupigia haupokei mkuu au ushapangisha nini?
Hahahahaha hapo si bora uishi mwenyewe na mama nanihii
mkuu yaani maisha ya bongo ni utapeli mtupu. Hivi hii nchi ina mcha Mungu kweli ukitoa watoto wadogo. Maana vipato na matumizi ya watu haviendani kabisa.
Unakuta kalani wa mahakama ya mwanzo amempangia nyumba ndogo hapo bado bili za umeme na maji, chakula, usafiri, vinywaji, kujiremba n.k
nchi hii hakuna wala rushwa wakubwa kama watumishi wa mahakama. Nilikuwa najiuliza kila siku kwa nini vijana wengi wanakimbilia kusoma sheria au kwenda kusoma Lushoto chuo cha usimamizi wa mahakama, kumbe wanajua ukitoka huko unanyookewa milele mradi uajiriwe tu. Makarani, mahakimu na majaji nchi hii hakuna msafi hata mmoja.
Kuna mmoja alikuwa pale kimara mahakama ya mwanzo kama hakimu inasemekana kwa siku alikuwa anatoka na pesa nyingi sana. imagine hakimu mahakama ya mwanzo ana nyumba kadhaa hapa mjini za kupangisha, ana simu za nguvu, anaishi kijitonyama kwenye nyumba yake mwenyewe, watoto wake wa kike wanasoma Marian girls bagamoyo-ada kwa mwaka 1.2ml plus na pengine anao wawili au watatu au wako aga khan mzizima. na ana daladala kama nne hivi coaster-Japan, na amenunua zote kwa mkupuo..................... na pay slip yake inasomeka tsh 260000
Hakuna sheria inayomkataza mtu kuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja. Nadhani ili halina marumbano. Mtu mmoja anaweza kuwa na vyanzo zaidi ya mia moja vya mapato.
Matharani, kuna mtumishi mmoja wa serikali ambaye naye analipwa mshahara wa sh 500,000. Mtumishi huyu ana duka hapo nyumbani kwake, ana genge la nyanya, vitunguu, matunda na mboga mboga. Amefuga ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kuku wa nyama na mayai, ana guest house, ana nyumba moja ya kupangisha ambayo mbele yake ina frem za maduka ambayo nayo anayapangisha. Ana vijibaiskeli vya kusambaza maji kawapatia vijana ajira , ana baba shop ya kunyoa manywele n.k.. Mkewe nyumbani anapika maandazi, vitumbua na chapati anasambaza katika migahawa.Huyu jamaa ana vyanzo visovyopungua kumi ninavyovijua mimi. Huyu ni mtu hodari na mchapakazi kweli kweli. Anatoka mikoa ya kaskazini, anaishi Mbezi ya shamba. Ukienda kumtembelea nyumbani kwake unakutana ana kwa ana na shombo la mifugo kama una-aleji nalo unaweza kuondoka bila kusema bai bai! Lakini yeye na familia yake wamelizoe kama wale jamaa wanaoishi kandokando ya dampo la kigogo. Majira zake hawlipendi hilo shombo wanapenda maziwa,mayai na nyama, maana huyu jamaa kila ifikapo siku kubwa lazima achinje! Wewe una vyanzo vingapi vya mapato? Kama unachokimoja tu cha huko Sirikalini, ushauri wa bure fungua banda la chips mayai hapo mtaani kwenu maana wakazi wa Dar hawapendi wugari! wanataka sana rede medi chips mayai zilizoandaliwa na mafuta ya koreeeeea!