Hakuna sheria inayomkataza mtu kuwa na vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja. Nadhani ili halina marumbano. Mtu mmoja anaweza kuwa na vyanzo zaidi ya mia moja vya mapato.
Matharani, kuna mtumishi mmoja wa serikali ambaye naye analipwa mshahara wa sh 500,000. Mtumishi huyu ana duka hapo nyumbani kwake, ana genge la nyanya, vitunguu, matunda na mboga mboga. Amefuga ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kuku wa nyama na mayai, ana guest house, ana nyumba moja ya kupangisha ambayo mbele yake ina frem za maduka ambayo nayo anayapangisha. Ana vijibaiskeli vya kusambaza maji kawapatia vijana ajira , ana baba shop ya kunyoa manywele n.k.. Mkewe nyumbani anapika maandazi, vitumbua na chapati anasambaza katika migahawa.Huyu jamaa ana vyanzo visovyopungua kumi ninavyovijua mimi. Huyu ni mtu hodari na mchapakazi kweli kweli. Anatoka mikoa ya kaskazini, anaishi Mbezi ya shamba. Ukienda kumtembelea nyumbani kwake unakutana ana kwa ana na shombo la mifugo kama una-aleji nalo unaweza kuondoka bila kusema bai bai! Lakini yeye na familia yake wamelizoe kama wale jamaa wanaoishi kandokando ya dampo la kigogo. Majira zake hawlipendi hilo shombo wanapenda maziwa,mayai na nyama, maana huyu jamaa kila ifikapo siku kubwa lazima achinje! Wewe una vyanzo vingapi vya mapato? Kama unachokimoja tu cha huko Sirikalini, ushauri wa bure fungua banda la chips mayai hapo mtaani kwenu maana wakazi wa Dar hawapendi wugari! wanataka sana rede medi chips mayai zilizoandaliwa na mafuta ya koreeeeea!