House4Rent Nyumba inapangishwa (vyumba vitatu)kimara baruti

House4Rent Nyumba inapangishwa (vyumba vitatu)kimara baruti

Tunzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
4,082
Reaction score
2,402
Nyumba ipo Kimara Baruti kutoka morogoro road ni dk 4 Ina vyumba vitatu vya kulala kimoja master bedroom sebule jiko pamoja na public toilet Ina Tailz jipsum na MAJI yanatoka ndani masaa 24 pia Ina madrisha ya aluminum ipo kwenye fensi ya kujitegemea kodi laki tano mwezi (500000)ilipwe miezi sita pia kuna mazungumzo kwenye miezi

Kwa maelezo nichek kwa 0684448888
IMG-20190103-WA0001.jpeg
IMG-20190103-WA0020.jpeg
IMG-20190103-WA0018.jpeg
IMG-20190103-WA0007.jpeg
IMG-20190103-WA0028.jpeg
IMG-20190103-WA0030.jpeg
IMG-20190103-WA0024.jpeg
IMG-20190103-WA0014.jpeg
IMG-20190103-WA0017.jpeg
IMG-20190103-WA0002.jpeg
IMG-20190103-WA0016.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeipenda kiasi, sio saaana kivile!!
But haijanishawishi mpaka nikubali baba Debo atoe laki tano kila mwezi.
Kasoro ya kwanza rangi kwenye fito za paa la nyumba imebanduka banduka.
 
inajitegemea ndani ya uzio.
 
Nimeipenda kiasi, sio saaana kivile!!
But haijanishawishi mpaka nikubali baba Debo atoe laki tano kila mwezi.
Kasoro ya kwanza rangi kwenye fito za paa la nyumba imebanduka banduka.

Mkuu umeshapata ile ya 150K kwa Dalali B? sasa nyumba ya 150k na 500k kuna ushirikiano hapo?
 
Nyumba iko fresh,mwenye uwezo wake achukue nyumba hio.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni nzuri sana.. na haipo mbali na barabara

Hutopata mteja nakwambia, kama utaendelea kupuuzia ushauri wangu.
Mwambie mwenye nyumba wako apake rangi ufito wa paa.
Utalala njaa, shauri yako.
 
Hutopata mteja nakwambia, kama utaendelea kupuuzia ushauri wangu.
Mwambie mwenye nyumba wako apake rangi ufito wa paa.
Utalala njaa, shauri yako.
Mkuu mimi sio mwenye nyumba, akija mteja akiipenda na akitaka hayo marekebisho anafanyiwa, na mm sitegemei hiyo nyumba! Hii hapa tu kwenye compound yangu nimeshakula kichwa! hapa mjini kuna nyumba nyingi, hapa baruti tu zipo zaidi ya 20! sembuse hiyo?
 
Hii ikizidi sana kwa mwezi labda 250k.. Zaidi ya hapo huwezi pata mteja
 
Nyumba nzur kias ila kwa hilo eneo kodi ya laki tano utachelewa sana kupata wateja ila atlist btn 350,000 - 400,000TZS
 
Pango 500K maeneo ya Baruti nyumba ya vyumba vitatu!
Mwambie mwenye nyumba apunguze kidogo.

Hiyo kwa hali ya sasa ametaka nyingi isizidi 300K. Pesa ngumu na huku Kimara Baruti sio Sinza, Mlimani City, Mikocheni, Msasani, Mwenge, K/nyama, Kinondoni, Magomeni, n.k.
 
Nyumba nzuri ndio ila marekebisho madogo sana kwenye paa japo haipendez kumpangia bei aliyeijenga endapo ataona hapati wateja I hop atashusha from 500K to 300K or 400k
 
Nimeipenda kiasi, sio saaana kivile!!
But haijanishawishi mpaka nikubali baba Debo atoe laki tano kila mwezi.
Kasoro ya kwanza rangi kwenye fito za paa la nyumba imebanduka banduka.
Laki 5 kimara baruti? Kwa usawa huu hupati mpangaji eti ulipe miezi 6 thubutuuu
 
Hii ikizidi sana kwa mwezi labda 250k.. Zaidi ya hapo huwezi pata mteja
Pole sana mkuu ila hii nyumba kwa bei hiyo hapana!.. mm kama dalali kwa nyumba hiyo mwisho 450,000 japo mm mwenye nyumba akiamua kuchukua 250k mm nitafurahi koz wateja hao wapo kibao.. ila nakuambia demand ya vyumba vitatu nikubwa.. hii haimalizi j2 jioni imeshaondoka
 
Laki 5 kimara baruti? Kwa usawa huu hupati mpangaji eti ulipe miezi 6 thubutuuu

Pole mkuu wapo wanaolipa hiyo! kila mtu na uwezo wake! kumbuka ile niliyoitangaza ya barabara ya chuo! 500k haikumaliza siku mbili, na bado nina watu kibao ndio mana nikapambana nikapata hii, Na hii sema wateja wangu ndio kama nyie! wengine ndio kama hivyo wanataka 450k ila mwenye nyumba yupo radhi apunguze miezi.. leo na kesho huikuti, mana kuna madalali wateja wao wako na uhitaji wa kweli na wako njema
 
Nyumba nzuri ndio ila marekebisho madogo sana kwenye paa japo haipendez kumpangia bei aliyeijenga endapo ataona hapati wateja I hop atashusha from 500K to 300K or 400k

Anapunguza miezi ila sio bei! Na ukweli ni kwamba hii wkend na mpambambo ninaouona wa madalali wengine wenye wateja wa uhakika soon nitasema imepangishwa
 
wenye uwezo wa kulipa kodi mil 3 kwa miezi 6 wameshajenga mijengo yao kitambo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu inaonakana kuna aina ya nyumba ulizozizoea ndio mana hii ya 500k inakupa tabu, basi si kwa ajili yako, watu wanalipa $1500 mpaka 3000$ kwa mwezi na zaidi nyumba za kuishi sembuse hiyo?
Kwa hayo mawazo yako inaelekea huwezi kua jirani yangu!
 
Back
Top Bottom