House4Sale Nyumba inauzwa, ipo Tabata Relini barabarani. Bei nafuu kabisa

Dalali msomi. Umesomea taaluma gani mkuu ?

Acha kukaa kihasara hasara
 
Kiongozi hili eneo la nyumba halijai maji wakati wa mvua?
Iko eneo zuri sana ila nimeuliza hivyo kwa sababu moja nimeona hiyo nyumba imechanika
1.Nyumba iko bondeni,
Kwa hizo picha inaonekana kabisa kuta zimeloa mpaka madirishani afu Unasema ENEO HALIJAI MAJI.

2. Hiyo barabara ya rami inaonekana Haina Mfereji wa maji afu nyumba imeisogelea kabisa lami.
Maana ake umejenga kwenye hifadhi ya barabara.

3. Umesema NYUMBA iko relini, hapa sijui unajenga kitu gani kwny Akili ya MTEJA. Ukizingatia kipaumbele Cha awamu ya 5 Ni SGR na RAISI keshasema itapita hapo.

YOTE KWA YOTE, nakutakia biashara njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiachia kuhusu reli pia mnunuzi anatakiwa ajiridhishe na upana wa barabara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo halina Shaka kabisa kua imejengwa barabarani kabisa
(sio Tena kwny hifadhi ya barabara)

Kwa maana Hamna Rami inajengwa bila mifereji ya kupitishia maji.

Ukiiangalia hiyo lami Haina mifereji ya maji, maana ake jamaa alijenga kwenye eneo la Mfereji wa maji.

Kesho TU,
PANABOMOLEWA KUPISHA SGR au utanuzi wa barabara


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elfu 15 ipo chap tumalize biashara nipageuze gesti bubu, shoo time buku mbili dakika 10
 
Bosi ulikuwa una haraka ya nini sasa,si ungesubiri tu angalau hizi alama za mafuriko zinazoonekana hadi madirishani zikauke!..ungeuza kwa bei nzuri nakwambia. Sasa umeshaharibu kabisa manake kabla ya kununua nawaza kifusi cha kujaza mpaka level ya mabati hapo kisha ndio nianze kujenga msingi....nakushauri usiuze manake utampa presha mnunuzi asijeondoka na upepo wa Kisulisuli bure..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…