Nyumba na. 81 Aggrey street Dar es salaam 1955

Abunuwasi,
Allahuma Amin.

Sasa chepuka kidogo hapo ingia Kisutu mjini kwenyewe.
Pata na picha ya Msikiti wa Mwinyikheri ule wa zamani.
 


Nimevutiwa na ustaarabu wako basi ntafurahi kuziona mada zako nyingi zina mafunzo hasa kwa namna unavyoandika lugha yetu ya kiswahili inavutia sana nakupongeza sana.
 
Nimevutiwa na ustaarabu wako basi ntafurahi kuziona mada zako nyingi zina mafunzo hasa kwa namna unavyoandika lugha yetu ya kiswahili inavutia sana nakupongeza sana.
Radika,
Ahsante kaka.
Nimezaliwa na kukulia Dar es Salaam Kariakoo ya 1960s.
Sina ''vernacular,'' ninasema Kiswahili toka utoto.

Ingia: www.mohammedsaid.com
 
Nashukuru mkuu ngoja nicheki.
Radika,
Karibu.

Unaweza kufanya ''search,'' kwa majina na matukio.
Mathalan Julius Nyerere, Rashid Kawawa, TANU, Mapinduzi ya Zanzibar nk.

Ukiingia kwenye ''Gallery,'' kuna DVD na Audio nazungumza.
 
Radika,
Karibu.

Unaweza kufanya ''search,'' kwa majina na matukio.
Mathalan Julius Nyerere, Rashid Kawawa, TANU, Mapinduzi ya Zanzibar nk.

Ukiingia kwenye ''Gallery,'' kuna DVD na Audio nazungumza.



Shukrani sana kwa ufafanuzi nitafanya hivyo.
 
Zitaletwa za Matonya mwishowe,kule Yombo alikuwepo mgogo mmoja anauza matunda,miwa nk akijiita bonyebonyeee,siju bado yupo hai!
 
Bali...
Ahsante kaka.
Mkuu nakukubali sana,nataka nikitulia nitafute muda,nawe ukubali kunipa wasaa,nikutembelee unijuze ilimu,wajua sisi hatukubahatika kuwa karibu na watu wanoijua nchi hii ,hivyo kazi kwetu kuitafuta kwa wajuzi kama wewe ,maalimu
 
Ni kweli kabisa na kila mtu mzima alikuwa ni mzazi pia kwani aliweza kumuadibisha mtoto yoyote aliyekosa mahapa popote pale anapoona inafaa.
Na ikitokea baada ya hapo akamhadithia mzazi halisi basi kesi na adhabu huanza upya kabisa.

Duh Abunwasi umenikumbusha mbali sana.
Juzi nilikuwa katika mikutano yangu ya biashara nikaulizwa nielezee nilikulia katika mazingira gani utotoni.Nilijibu Kama ulivyo elezea hapo juu Na nikaongezea Nilikuzwa na kulelewa Na mtaa mzima. Maana toka natoka nyumbani mpaka shule ninachungwa Na majirani bila ya kujijua.Nikigombana Au nikafanya utovu wa Nidhamu nitapigwa Au kukemewa Na wazee wa mtaani.Kwa kweli huwa namshukuru Mwenye-EZ-Mungu Kwa mapenzi ya majirani Na Watu wengi tu.Naongelea miaka ya 60s Na 70s
 
Bro,
Ndiyo maana tuko tulivyo kwani tuliokwa vizuri na hadi leo hata matusi toka midomoni mwetu inakuwa ni vigumu sana.
 

Ndungu yangu Mtebetini inshaalah nitakutafuta mwezi ujao(wa 10) tukutane.ni takuPM
Panapo majaaliwa.
 
mzee@mohamed said makala zako huwa zinanivutia ila huwa sipati funzo lolote kwenye hizo habari. Naomba nisaidie lengo la visa vya kihistoria unavyotupatia ni kutusaidia kupata funzo gani. Mfano kisa hiki kinatufunza Nini, na je ulitaka DSM za enzi ya 1950 ibaki vilevile na ili iweje
 
Lutayega,
Sababu ya kuweka post hiyo ni kuonyesha Dar es Salaam ilikuwaje.
Hii ni katika kuhifadhi historia kwa vizazi vijazo.

Visa kama ulivyoita ninavyoweka ni kueleza mambo ambayo si wengi
wanayajua na kwa sababu ile ile ya kuhifadhi historia.

Kuhusu kupata funzo hiyo inategemea na inatofutiana kati ya mtu na
mtu.

Kuna wanaopata elimu mpya katika makala zangu na kuna wengine
wanatoka hawajaelewa kitu.

Sijui nini kimekufanya useme kuwa natamani Dar es Salaam ingebaki
kama ilivyokuwa.
 
asante kwa ufafanuzi, kilichonifanya kukuliza nimeona kwenye Maelezo yako kama unalalamika eneo ilipokuwapo hiyo nyumba kujengwa magorofa.
 
asante kwa ufafanuzi, kilichonifanya kukuliza nimeona kwenye Maelezo yako kama unalalamika eneo ilipokuwapo hiyo nyumba kujengwa magorofa.
Lutayega,
Mimi sijalalamika popote.
Nimeleeza tu hali ilivyo hivi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…