Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Darcity,Allah amekujaalia busara, inshaallah na ailinde.
Allahuma Amin kwa sote.
Nawe pia utapata busara In Shaallah utakapofika makamo yangu.
Uzee dawa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Darcity,Allah amekujaalia busara, inshaallah na ailinde.
Tusker...Asante sana kwa Historia iliyotukuka Mzee wetu. Tunaomba uendelee kuiweka humu kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Asante sana.
Watu sasa wanayao kila mtu ana ghadhabu zake,wala usiliweke moyoni,....wanasema ukubwa jalala.Isambe,
Ahsante ndugu yangu.
Nimeshangazwa na ile chuki katika kauli zake.
Nimejiuliza kipi kimemghadhibisha huyu ndugu yangu?
Yawezekana katika ile ''post,'' lipo kosa nami sikuliona.
Ikiwa hivyo ndivyo ilikuwa yeye kunielekeza basi nami
nitoe jibu.
Lakini anakuja na ghadhabu na matusi pasi na sababu.
Maalim wangu salaam aleykum, mi nilikutana na Juma Kubbe juzi msikiti wa Mwembe chai kwenye kisomo cha tahtim ya Marehemu Bi Tatu Mrisho mke wa Rahim Lumelezi aliyekuwa mchezaji wa Simba Sports Club basi Sheikh Thabit alimwita kwa jina lake la utani Jimmy Lover nilimuona Juma kubbe akitabasamu kama hulka yake ilivyo siku zote ni mtu wa kutabasamu na mas'hara sana.Tusker...
Kila inapotokea nafasi In Shaallah nitajaribu kueleza kile ninachokifahamu.
Juma kubbe na mtaa Stanley Aggrey habanduki kwenda kukote alipisha ujenzi wa ghorofa uishe karudi hapo hapo mpaka leo! Nyumba yao ya miaka ya nyuma ilikuwa nyumba no.74 na Mzee wake marehemu Mzee Khamisi Kubbe Msukuma mjanja aliyekuwa akitengeneza vifaa kama ndoo za bati,sufuri,koroboi,machekeche na vinavyohusiana na mabati hapo nyumbani kwake kabla ya kuhamia Gerezani,nimemwita mjanja kwa sababu alikuwa na soko la kuuza vifaa hivyo mpaka Mwanza zama hizo za miaka ya sitini!.Tusker...
Kila inapotokea nafasi In Shaallah nitajaribu kueleza kile ninachokifahamu.
Allah akbar. Sheikh nasubiria kwa hamu hilo andiko.Slim5,
Ahsante sana.
Kulikuwa na somo yako hapa Dar anaitwa Slim.
Alikuwa mtu wa mikasa kweli kweli.
In Shaallah iko siku nitaleta visa vyake hapa barzani.
Kama Dar ya 1970 kulikuwa na wajanja 10 na yeye
namba yake imo humo tena nafasi za matawini.
Mtebetini,Juma kubbe na mtaa Stanley Aggrey habanduki kwenda kukote alipisha ujenzi wa ghorofa uishe karudi hapo hapo mpaka leo! Nyumba yao ya miaka ya nyuma ilikuwa nyumba no.74 na Mzee wake marehemu Mzee Khamisi Kubbe Msukuma mjanja aliyekuwa akitengeneza vifaa kama ndoo za bati,sufuri,koroboi,machekeche na vinavyohusiana na mabati hapo nyumbani kwake kabla ya kuhamia Gerezani,nimemwita mjanja kwa sababu alikuwa na soko la kuuza vifaa hivyo mpaka Mwanza zama hizo za miaka ya sitini!.
Mtebetini,Maalim wangu salaam aleykum, mi nilikutana na Juma Kubbe juzi msikiti wa Mwembe chai kwenye kisomo cha tahtim ya Marehemu Bi Tatu Mrisho mke wa Rahim Lumelezi aliyekuwa mchezaji wa Simba Sports Club basi Sheikh Thabit alimwita kwa jina lake la utani Jimmy Lover nilimuona Juma kubbe akitabasamu kama hulka yake ilivyo siku zote ni mtu wa kutabasamu na mas'hara sana.
Ni kweli kabisa na kila mtu mzima alikuwa ni mzazi pia kwani aliweza kumuadibisha mtoto yoyote aliyekosa mahapa popote pale anapoona inafaa.Othiambo,
Hakika nyakati zile wazee wakituhimiza sana kuhusu adabu.
Walikuwa na neno lao wakituasa,''Usitutukanishe.''
Maana ikiwa mtoto atakosa adabu watu watajua mama yake
hakumfunza adabu na hili kwao lilikuwa tusi kubwa.
Ustaarabu bado ungalipo ni wajibu wetu kuwafunza wanetu
na hata hapa barzani ikiwa unahisi mtu hakupata malezi kwao
kwa njia ya utaratibu unamuelekeza kuwa huenda huko kwenu
si vibaya lakini haifai kufanya kadha wa kadha kwenye kadamnasi.
Abunuwasi,Ni kweli kabisa na kila mtu mzima alikuwa ni mzazi pia kwani aliweza kumuadibisha mtoto yoyote aliyekosa mahapa popote pale anapoona inafaa.
Na ikitokea baada ya hapo akamhadithia mzazi halisi basi kesi na adhabu huanza upya kabisa.
Clint Eastwood????Abunuwasi,
Sisi tulikuwa tunakatazwa kwenda kuogelea pwani.
Wazee walikuwa wanahofu tusije tukazama.
Lakini tukienda kuogelea kwa siri sana na pale ilipo
ofisi ya Azam Marine kulikuwa na pipa la maji baridi.
Tukishatoka kuogelea tunakuja pale kuoga katika lile
pipa kuondoa chumvi ili nyumbani tusijulikane.
Kazi ilikuwa wakati wa kurudi tusikutana na mtu akenda
kusema katuona Uzunguni.
Kule kote kulikuwa kunaitwa, ''Uzunguni.''
Ikiwa tutamuona mtu anatufahamu kwa mbali tulikuwa
tunajificha.
Lakini kama ujuavyo siku za mwizi 40.
Tulipotimia umri wa kati tuko sekondari ''past time,'' kubwa
ilikuwa ''movies'' Empire Cinema mchana Jumamosi na Jumapili.
Tukiangalia, ''Westerns.''
Hii wazee wenyewe wakifurahi unapewa shilingi moja na senti
ya soda ila unakumbushwa kurudi nyumbani mapema.
Abunuwasi,Clint Eastwood????
Maalim wangu umenifanya nimkumbuke marehemu Baba yangu kwa kuwataja hao wababe wa classic movies,kuna One Silver Dollar,Seven dollars to kill you. Mimi pamoja na kuwapenda hao kipenzi changu mwingine alikuwa Charles Bronson.Abunuwasi,
''The Good, The Bad and The Ugly...'' my all time favourite Western.
Giuliano Gemma, Anthony Stefen, Ferdinando Sancho...
Umenipeleka mbali sana.
Hapa kwangu nina projext size ya mkono.
Usiku ''sitting room,'' yangu huwa ''theater'' nina ''classics,'' nyingi na sichoki
kuziangalia - ''Lawrence of Arabia,'' ''The Guns of Navarone,'' ''Blue Hawaii,''
Elvis huyu.
Hii movie niliiona siku ya Eid Fitr Empire 1964 nilikuwa na miaka 12.
Ndipo nilipoamua kujifunza kupiga guitar na kuimba.
Zingine nikiziangalia na marehemu baba yangu katika 1960s...
Huwa narudi nyuma sana utotoni niko kizani peke yangu najihisi niko
Empire.
Nikipenda pia kusoma ''comics'' nilipokuwa mtoto kisha novels nilipopata makamo.
Mtebetini,Maalim wangu umenifanya nimkumbuke marehemu Baba yangu kwa kuwataja hao wababe wa classic movies,kuna One Silver Dollar,Seven dollars to kill you. Mimi pamoja na kuwapenda hao kipenzi changu mwingine alikuwa Charles Bronson.
Bansen...Dunia inaenda kwa kasi sana..
Maalim umenipeleka mbali sana wakati nasoma Mombasa Kenya 1974 niliona “The Mechanic”Mtebetini,
My all time favourite ya Charles Bronson ni ''Chatoo's Land.''
You can say that Again and Again bro we were blessed to experience our childhood during that period. Unakumbuka ujanja wetu kwa wasichana uliishia kwenda kwenye buggy splendid new palace, anatoglo], movies,parties lakini hakukuwepo na pombe?? na mwisho wa yote tuliridhika kwa busu tu.Bansen...
Utadhani ilikuwa jana tu.
Namshukuru Allah kwa kunileta wakati ule...
Those were the days we thought would never end...
Hivi jamani mnamkumbuka mzee Mpangile pale kwenye makaburi ya kisutu ambaye wakati tukiwa wadogo tulikuwa tunakwenda kupopoe maembe maeneo yale naye alikuwa anatufurusha mbio ilikuwa kama mchezo wa paka na panya pale-Ni kweli kabisa na kila mtu mzima alikuwa ni mzazi pia kwani aliweza kumuadibisha mtoto yoyote aliyekosa mahapa popote pale anapoona inafaa.
Na ikitokea baada ya hapo akamhadithia mzazi halisi basi kesi na adhabu huanza upya kabisa.
Abunuwas,You can say that Again and Again bro we were blessed to experience our childhood during that period. Unakumbuka ujanja wetu kwa wasichana uliishia kwenda kwenye buggy splendid new palace, anatoglo], movies,parties lakini hakukuwepo na pombe?? na mwisho wa yote tuliridhika kwa busu tu.