Nyumba Ndogo Mlaaniwe!!

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,602
Reaction score
5,809
Naja mbele yenu. Majuto ni mjukuu. Nyumba ndogo, hawara ama mpango wa Kando. Naja kuwalaani:

1. Mmenifanya nimdharau mke wangu. Mke wangu ameishi kwa masikitiko na manyanyaso yote ni sababu yenu.

2. Familia yangu nimeitekeleza. Kila nikitakiwa kutoa pesa najiona kama naonewa, si jukumu langu tena. Imekuwa kama natoa msaada. Mmenifanya nini nyie viumbe mliolaaniwa.

3. Mmeichukua Furaha ya Familia yangu. Sina muda wa kukaa na familia yangu. Mmenifunga na kufungik. Nyie viumbe mso na Huruma.

4. Mmenimiliki kama Asset yenu. Akili yangu mmeishika ikashikika. Nimeshindwa kuwekeza chochote, pesa zote mmezifyonza kama Viwavijeshi wanavyokula Shambani. Kuweni na huruma. Ihurumieni familis yangu. Mungu yupo awalaani.

Hivi kweli mnamjua mungu kweli. Mmeshindwa kuionea hurum familia yangu, mmeshindwa kuwaonea huruma watoto wangu wanavyopata tabu. Kila mkiniona na senti mnajifany mna hamu, kumbe ni ili mniikwapue.

Penzi lenyewe la kupimiwa kama umeme wa Luku. Haupatu hadi ujaze fomu ya maombi.

Mungu awalaani hadi mshangae!!
 
Wamekupata vipi? au ulianza kuwatafuta ukajikuta at a point of no return... kwanza inabidi usomewe ujikwamue nao halafu ndio uanze kuwapa laana kama bado unao laana haifiki....
 
na bado mkikosa mnaanza kuwaambia wakezenu,Mke wangu siku hizi sipati hela.honey zinakua kibao,wakati mnazo badala ya kusave na kuwekeza nyie mnahonga,utajamba cheche
 
Ningeshangaa usinge comment hii sred
na bado mkikosa mnaanza kuwaambia wakezenu,Mke wangu siku hizi sipati hela.honey zinakua kibao,wakati mnazo badala ya kusave na kuwekeza nyie mnahonga,utajamba cheche
 
Anaugua huyu mzee hajui smal house wanarun dunia
 
Ha ha ha amhonge nani?mie nahonga bana kwani uwezo ninao hua nahitaj mshedede2 sometimes pesa kwangu si ishu
small house haya mtu wako huyo.msaidie mpe mtaji,alikuhonga nyingi mno
 
Last edited by a moderator:
Wamekupata vipi? au ulianza kuwatafuta ukajikuta at a point of no return... kwanza inabidi usomewe ujikwamue nao halafu ndio uanze kuwapa laana kama bado unao laana haifiki....

Kujivua gamba nimeshindwa. Wananiona kama Boya. I love you nyingi kumbe za wizi.
 
na bado mkikosa mnaanza kuwaambia wakezenu,Mke wangu siku hizi sipati hela.honey zinakua kibao,wakati mnazo badala ya kusave na kuwekeza nyie mnahonga,utajamba cheche

Huo sio ushauri ni kashfa sasa. Kujamba cheche ina maana gani sasa.
 
Mzee kwani walikubaka?? au walikuendea kwa sangoma??
 
Last edited by a moderator:
Huo sio ushauri ni kashfa sasa. Kujamba cheche ina maana gani sasa.
Hujui utajua tu,siku utakapofikisha miaka 65 kama ukibahatika,hujasomesha wanao,umeshastaafu kama ulikuwa unafanya kazi,mafao umekula na una watoto kila mtaa,wakati MUNGU anakubariki wewe ni kuhonga tu siku hiyo ndo utaisoma number kwa kiebrania
 
amu imekugusa. Mnatufanya kama hatuna akili.

mie ckatai nyumba ndogo kweli na hakikisha watoto wanakula kabla mie na baba yao hatujasosomola manyama.
Tatizo lako nyumba ndogo yako inaendesha mambo kiswazi.
Ukimpata msomi wa kidijital kama mie usingekuja kulalamika home
 
Last edited by a moderator:
Mzee ulikosea kidogo hukusoma "the guide" nenda kule chit chat ipo kule tafuta uzi wa The Boss
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…