Nyumba ninayoishi inasemwa kuwa ina mauzauza sana lakini sijawahi kuyaona

Hata hivyo Watanzania mnapenda sana uzushi.

Anaweza kutokea mtu mmoja tu akajitungia kitu; basi, kila mmoja anakuwa balozi.

Mfano: Mtu anaamua kusema kule sumbawanga kuna wachawi. Basi kila mtu huamini kila anaetoka Sumbawanga ni mchawi.
Mbona mimi naamini wewe ni shetani au nimedanganywa?
 
Endelea na maisha na omba punguzo la Kodi kwa ajili ya kuishi nyumba wanayo kimbia wapangaji
Baba mwenye nyumba anaelewa ...kila nikimuomba anivumilie nimekwama huwa anaelewa kwa haraka sana
 
Nimewahi kuishi maeneo na nyumba kadhaa yanayosemekana kuwa na mambo kama hayo, niliishi comfortably sijawahi ona hizo mambo zaidi ya wenzangu
Kuna nyumba unasikia kwa watu..
kuna nyumba mauzauza yapo live
unalipa kodi miezi 6 unahama baada ya siku 3 unakimbia unasamehe na kodi!
 
Kuna nyumba unasikia kwa watu..
kuna nyumba mauzauza yapo live
unalipa kodi miezi 6 unahama baada ya siku 3 unakimbia unasamehe na kodi!
Wakinifila nahama lakin kama wanadili na mambo yao naishi nao milele
 
Wewe ndio uza uza lenyewe sasa
 
Mwili wako ni dhaifu ..hauna spiritual power ...kama chaji katika simu basi ujue ukifungua YouTube video ya dakika 5 simu yenyewe inazima ....

Muombe Mungu sana akuongezee chaji mwilini....
 
Nimeshalala kwenye nyumba moja wanadai ina mauzauza,uzuri kazi zangu nafanyaga usiku wa manane mpaka asubuhi,kwa muda wa miezi mitatu nilikuwa nasubiri hayo mauzauza sikusikia wala kuona chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…