Nyumba nzuri ya kisasa inauzwa Kijitonyama

Nyumba nzuri ya kisasa inauzwa Kijitonyama

dovillenproperty

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
3,203
Reaction score
2,227
Nyumba ipo kijitonyama Afrikasana na haiko mbali sana na shekilango road,na pia iko jirani na soko la Afrikasana.

Vyumba 4 self, nk

Size plot 400 sqm

Bei 300m

Maongezi zaidi 0756060183
IMG-20190516-WA0000.jpeg
IMG-20190516-WA0004.jpeg
IMG-20190516-WA0001.jpeg
IMG-20190516-WA0005.jpeg
IMG-20190516-WA0006.jpeg
 
Hahaha, eti 260m!!!! Asante mkuu. Tutaishi kama mashetani awamu hii ya tano
 
Wenye nyumba wa Dar, plot size 20m x 20m, bei ya "mjengo", 300M, yaani bado kidogo tu iwe theluthi bilioni!! Wengine tukielezea hii situation, kuna wengine wanadhani tunajifanya mambo safi kumbe tunazungumzia uhalisia! Yaani wenye nyumba Dar utadhani wanakesha na mmemea wanapoenda kulala!

c.c Allen Kilewella

Huyu anauza kiwanja 70mx70m kwa takribani Sh. bilioni moja, but it's understandable, sio beach bhana, tena Msasani! Sasa sijui kipimo chake kimezingatia eneo unalotakiwa kutojenga kutoka ufukweni
Beach.png
 
Nimesoma kwa kurudia rudia mara 3 zaidi ila nimeshindwa kuelewa maana yake
Wenye nyumba wa Dar, plot size 20m x 20m, bei ya "mjengo", 300M, yaani bado kidogo tu iwe theluthi bilioni!! Wengine tukielezea hii situation, kuna wengine wanadhani tunajifanya mambo safi kumbe tunazungumzia uhalisia! Yaani wenye nyumba Dar utadhani wanakesha na mmemea wanapoenda kulala!

c.c Allen Kilewella
 
myplusbee kwa "Exchange rate" ya dola kwa shilingi yetu kwa sasa nadhani hicho kiwanja ni sawa na shilingi bilioni mbili na milioni mia tatu (2,300,000,000).

Nisichokielewa ni kama kumbe bado kwenye fukwe ya Msasani kuna kiwanja chenye ukubwa wa 70* 70. Maana hiyo ni heka na kuwa na heka nzima msasani ambayo haijajengwa ni kazi kweli kweli.

Kwa mtazamo wangu bei ya nyumba na viwanja duniani kote hutegemea mambo mengi sana. Kwanza kabisa hali ya uchumi ya watu wa nchi husika, kuna suala la huhitaji kwa mnunuzi, umaarufu wa eneo linauzwa ama kupangishwa.

Umaarufu wa eneo una mambo mengine ndani mwake, kama vile urahisi ama ukaribu wa eneo, utulivu, mpangilio wa makazi na ukaaji wa eneo na jiorafia yake na hapa ni kutia ndani kama eneo liko karibu na bahari, mlima maarufu, eneo lisilopata mafuriko kiurahisi ama na uwepo wa huduma za kijami karibu.

Kwa vyovyote vile yale mambo ya "Majimatitu" yanafikirisha sana. Hivi kwa jiji kama la Darisalama ni lazima kweli watu wote watoke watokako waje Kariakoo ama Posta kwa ajili ya kufuata huduma za kijamii ama shughuli za kuwaingizia riziki?

Kuna uzembe mkubwa sana ulifanyika wa kutokupanga miji yetu hasa baada ya miaka ya themanini. Nakumbuka wakati Kijitonyama na Sinza zinapimwa na kuanza kujengwa, ilidhaniwa kwamba ni zoezi endelevu lakini halikuendelea.

Miaka ya tisini pia wakati Tabata Kimanga inapimwa wengine tukaona kama ni mwanzo mzuri wa kujenga mji mpya, lakini leo nenda tabata ukaone yale maeneo yaliyopimwa kwa matumizi ya umma yanatumikaje!!

Hivi inawezekanaje kuwa na miji midogo midogo ambayo haina huduma za kijamii na maeneo ya kuwafanya watu wapate riziki zao? Ndiyo maana kuna baa hadi kwenye makazi ya watu.
 
Umeongelea facts. Kuna kipindi serikali ilienda likizo watu wakawa wanajenga watakavyo. Kuja kurekebisha tena hiyo hali ni ngumu sana na inatakiwa fedha nyingi. Solution nzuri sana ilikuwa na kuanzisha Dar mpya maeneo ya eg Bagamoyo. Kuna nafasi kubwa na zoezi la kwanza lingekuwa ni upimaji wa upangaji wa Dar mpya. Gharama zinazotumika kuhamia Dodoma (kwa sababu mimi sioni sababu yoyote ya kuhamia Dodoma) zingekuwa kianzio. Dar mpya ingeunganishwa na Dar ya zamani kwa njia ya barabara (highway), train na Boti.
 
Mkuu Allen Kilewella,

Hilo eneo sio ekari moja bali ekari tatu na robo (according to Tangazo) na kwahiyo hata hesabu zangu za 70x70 kwa 1B hazikuwa sahihi kwa sababu nili-overlook na kudhani ni ekari 2 na robo!! Hata hivyo, I doubt kama hicho kiwanja kweli kina-exist. Kwanza nili-doubt uwezekano wa ekari 3 na robo kuuzwa $1 Billion Msasani! Aidha, nilipoiangalia kwa umakini hiyo pic, nikapata mashaka mengine kwa sababu Msasani naijua vizuri lakini nilishindwa kabisa kuwa na clue hiyo pic itakuwa Msasani eneo gani hasa kwa kuangalia hiyo beach elevation! Nilipo-dig more, nikakuta hiyo picha ni ya Malindi, Kenya!

Kwahiyo inawezekana ni kweli hicho kiwanja kina-exist lakini sio hiyo picha!

Tukirudi kwenye hoja yako ya msingi kabisa kuhusu mipango miji, ki ukweli Tanzania tuna serious problem. I don't care much about K'nyama ambavyo hatimae ilivurundwa, ikafuata Tabata na sasa Tuangoma ambako kote huko kulipimwa, kwa sababu kote huko ni vitongoji kwenye jiji ambalo tayari lilishavuruguka and nobody cares! Ninachoipendea Dar es salaam, contrary na sehemu kama Nairobi ni jambo moja! Unakuta kitongoji kila mtu kaangalia kwake-- huyu kaangalia kasikazini, jirani yake kaangalia mashariki! Jirani yake mashariki kaangalia kusini na jirani wa kusini kaangalia magharibi; yaani kila mtu na lwake lakini ukiangalia nyumba zao, zinakuwa mzuri!

Nimesema I care less about hili jiji ambalo kila mtu na lwake lakini hivi sasa naiangalia sana Dodoma! Akili ya Mtanzania itapimika vizuri zaidi kwa kuangalia Dodoma! Serikali ikishindwa kudhibiti ujenzi wa hovyo hovyo Dodoma, basi miji mizuri Tanzania tufanye subira tu, labda Yesu akisharudi, hapo huenda tukajali suala la ujenzi wa miji bora na iliyopangiliwa kisasa!

Sijawahi kufika Dom, labda wakazi wa huko wanaweza kuwa na clue ya mwelekeo wa Dodoma kuhusu suala zima la upangaji miji!

Tukija suala la kufuata social services city center kama vile K/koo, kwa kweli mambo mengine ni mazoea mabaya tu! Mimi nilikuwa sijapita Mbagala kwa muda mrefu sana lakini mwaka jana nikaenda kule! Ukiona mtu anatoka Mbagala kwenda K/koo kununua bidhaa, basi huyo atakuwa na matatizo manake nimeona almost everything pale Rangi 3 na Zakhem ambazo zipo pua na mdomo! Kuna biashara karibu zote! Kwa haraka haraka nimeona matawi ya benki zaidi ya matano pale, kuanzia CRDB, NMB. NBC, Kenyan Commercial Bank, Equity, nadhani na Diamond Trust Bank! Sasa mtu unaenda mjini kufanya nini! Mahali kama Tandika nako hivyo hivyo! Ingawaje Tandika ipo ndani ndani, na lakini kuna kila aina ya bidhaa tena kuzidi Mbagala kasoro matawi makubwa ya benki ukilinganisha na Mbagala!

Sina haja ya kutaja maeneo kama Ubungo, Magomeni, Manzese, Kimara, Kinondoni, K'nyama kwa sababu huko watu wengi wanakujua ukilinganisha na maeneo ya Temeke! Lakini ajabu, kote huko utakuta watu wanataka kwenda mjini ingawaje sehemu kubwa ya huduma zinapatikana huko huko! Mwisho saa kadha tu zilizopita sister angu kanipigia simu ya ku-cancel meeting yetu kwa sababu kaombwa na mother ampeleke K/koo kununua sijui madudu gani sijui! Mama anaishi Kijichi, ambako angeweza kwenda kwa urahisi kabisa Rangi 3 au Tandika lakini anataka K/koo!!

Binafsi siku hizi naweza kukata mwaka mzima sijakanyaga K/koo, kama ambavyo naweza kukata mwaka mzima sijakanyaga kwenye banking hall! Yaani endapo watu wengi wangekuwa kama mimi, I believe kule Posta na K/koo wangeonekana wale tu ambao hawana namna nyingine! Kwanza tangia iingie Jumia ndo kabisa! Hata siku nikichoka wali maharage, naingia tu Jumia Food wananiletea hadi ghetto! Yaani mi sipendi shida kabisa 😀 😀 😀 !!
 
Back
Top Bottom