Nyumba ya Ahmed Adam Adam aliyofikia Nyerere, Mikindani 1956 kukarabatiwa

Nyumba ya Ahmed Adam Adam aliyofikia Nyerere, Mikindani 1956 kukarabatiwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYUMBA YA AHMED ADAM ALIYOFIKIA JULIUS NYERERE MIKINDANI MWAKA WA 1956 WAKATI WA KUPIGANIA UHURU KUKARABATIWA NA SERIKALI

Historia ya nyumba hii nimeileza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Naweka hapa yale niliyoandika kuhusu nyumba hii:

"Julius Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili Mikindani kutoka Lindi siku ya Jumamosi.

Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote waliyokuwanayo uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza Nyerere.

Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo, aliyemiliki nyumba moja ya fahari.

Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na ilijengwa kwa mawe na chokaa.

Ahmed Adam aliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na ujumbe wake.
Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake.

Ilijengwa na hayati kaka yake Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza.
Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani.

Huenda alichukuliwa Misri mwishoni mwa mwa karne ya kumi na tisa na Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani wakati wa vita vya Maji Maji.

Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya Ujerumani na kwa kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo.

Katika Vita Kuu ya Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza. Baada ya vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita, Waingereza waliitikadi nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya Kiingereza na kwa hiyo ilibidi itaifishwe.

Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika na kwa ajili hii haikuweza kukosa kuhusudika.

Utawala wa Waingereza ulikuwa katika taratibu ya kuitaifisha nyumba hiyo wakati ilipofahamika kwamba serikali isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ya kifungu cha sheria ambacho kilisema kuwa mali ya Waafrika waliokuwa wakitumika katika majeshi ya watawala wao haiwezi kutaifishwa.

Hii ilinusuru nyumba hiyo na hivyo ilibakia mikononi mwa mwenyewe mpaka alipofariki na nyumba hiyo ikaja kuwa katika miliki ya mdogo wake, Ahmed Adam.

Ahmed Adam alikubali kumpokea Nyerere na ugeni wake nyumbani kwake.
Nyumba hiyo ilikuja kuwa tawi la kwanza la TANU Mikindani.

Siku hiyo hiyo ya Jumamosi, usiku Nyerere aliitisha mkutano na wanachama kama thelathini hivi walihudhuria.

Nyerere aliwaeleza kwa ufupi juu ya ile safari yake ya Umoja wa Mataifa na hali ya siasa kwa ujumla mjini Dar es Salaam.

Nyerere aliwahakikishia wasikilizaji wake kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Tanganyika itakuwa huru katika uhai wao."

1624125639510.png
 
Back
Top Bottom