Nyumba ya biashara yenye wapangaji wengi ni sawa na biashara ya umachinga

Nyumba ya biashara yenye wapangaji wengi ni sawa na biashara ya umachinga

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Unapojenga nyumba unakuwa na kusudio la ujenzi huo. Hii inakusaidia kupata ramani na budget ya jengo. Wengi wetu baada ya kujenga nyumba ya kukupatia vijusent kwakua nyumba ni asset inayodumu.

Katika maongezi kuna mwekezaji wa nyumba za biashara aliyeniambia, ukijenga nyumba ya vyumba sita yaani vitatu vinavyoangaliana ndani, yaani choo bafuu jiko na nyumba viwili vya ziada. Ni rahisi kupata wateja.

Nimekitafakari hili wazo, ni kweli nyumba za aina hii mara nyingi zinajitangaza zenyewe. Mteja akihama wa chumba cha pili anaweza kumfahami mtu anaetafuta. Mwisho wa mwezi una uhakika wa kupata kodi kwani wateja ni wengi. Si wote hawatakuwa na pesa za kukupa.

Changamoto ni kukusanya watu wa tabia tofauti. Kuna ambao kuishi kwenye nyumba ya kupanga ndiyo wamepata freedom. Mziki utapigwa mpaka sauti ya mwisho redio si ya kwake bwana.

Mkusanyiko wa uchafu, maana vyumba sita wakiwa na familia mnaweza kuishi wato 30 nyumba moja. Ni muhimu kuwa na utaratibu unaofaa wa kukusanya na kutupa uchafu.
 
Back
Top Bottom