carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Cheshire, England. Nyumba ya nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, imevamiwa na wezi wakati kiungo huyo akiwa nchini Italia kwa mchezo ambao timu yake ilifungwa mabao 4-1 na Como, jana Jumatano usiku.
Taarifa ya Polisi wa Cheshire imethibitisha kuwa vitu kadhaa viliibwa katika nyumba hiyo iliyopo Nether Alderley, eneo la Cheshire, huku uchunguzi ukiendelea kubaini wahusika wa tukio hilo.Tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:30 usiku, Oktoba 21, 2026, wakati Fernandes akiwa na timu yake nchini Italia.
“Maofisa walifika eneo hilo lakini hawakuwakuta washukiwa. Hata hivyo, walibaini kuwa nyumba hiyo ilikuwa imevamiwa na vitu kadhaa viliibwa,” imesema sehemu ya taarifa ya polisi.
Polisi wanaendelea kupitia picha za kamera za usalama (CCTV) kutoka katika maeneo jirani ili kuwabaini waliohusika wa tukio hilo.