Nyumba ya kufunika kwa zege

Nyumba ya kufunika kwa zege

Mmeme

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2017
Posts
700
Reaction score
298
Nimetia nia kujenga nyumba ya kufunika kwa zege. Lakini kwanza kuna mambo nataka kufamu kutoka kwenu:

Je, kufunika kwa zege na kupaua kwa bati lisiloonekana, gharama zake zikoje kwa kulinganisha?

Je, ubora wa kuta za boma la kufunika kwa zege ni sawa na ule wa kufunika kwa bati?

Tofali za 5" (in 5) zinafaa kutumia kwa nyumba ya kufunika kwa zege?

Msaada wenu tafadhali.
 
Ni bora ukatumia tofali za nchi 6 ili utumie tofali chache. Katika ujenzi wa slab, gharama kubwa ipo kwenye nondo na cement. Probably kupaua kwa mfumo wa bati lisiloonekana ni nafuu zaidi kwa sababu idadi ya mbao zinazotumika ni chache.
Asante mkuu, nitayatilia maanani maoni yako.
 
Uamuzi wa kufunika paa kwa zege ulipaswa kuwa nao wakati wa kuchimba na kusimamisha msingi...otherwise msingi wa nyumba hauta himili paa la zege
Nashukuru mkuu kwa tahadhari uliyonipa.
 
20.jpg
20.jpg
kama hizi siyo ila nasikia siyo rafiki wa maeneo yenye mvua nyingi ila mwenyewe nazipenda
 
Una uhakika hii nibslab au mwarabu karudisha utumwa.
 
View attachment 1665872View attachment 1665872kama hizi siyo ila nasikia siyo rafiki wa maeneo yenye mvua nyingi ila mwenyewe nazipenda
Hizi nyumba lazima kumpata anayejua kupaua vizuri lasivyo utapata matatizo mbeleni,kuna jamaa namjua inamsumbua sana inavuja kula mvua ikinyesha.

Pia nyumba hizi zinahitaji finishing ya nguvu ujiweze kiuchumi utengeneze mazingira yawe vizuri,lasivyo nyumba itaonekana kama banda la kuku.
 
Hizi nyumba lazima kumpata anayejua kupaua vizuri lasivyo utapata matatizo mbeleni,kuna jamaa namjua inamsumbua sana inavuja kula mvua ikinyesha.

Pia nyumba hizi zinahitaji finishing ya nguvu ujiweze kiuchumi utengeneze mazingira yawe vizuri,lasivyo nyumba itaonekana kama banda la kuku.
Itavuja vipi wakati nimefunika kwa zege? Au sijaeleweka mkuu?
 
Uamuzi wa kufunika paa kwa zege ulipaswa kuwa nao wakati wa kuchimba na kusimamisha msingi...otherwise msingi wa nyumba hauta himili paa la zege
Samahani niko nje ya mada je ninapotaka kujenga nyumba ambayo itakua na kagorofa kamoja au tuwili inapsawa lazima site kuwe na mkandarasi au fundi anaeaminika anaruhusiwa?
 
Itavuja vipi wakati nimefunika kwa zege? Au sijaeleweka mkuu?
Zege ni ghali zaidi kama unataka kuokoa gharama. Pia zege ukiezekea lazima juu yake uweke material ya water proof vinginevyo likinyonya maji wakati wa mvua nyingi utakuja kukuta linavuja na litakuwekea alama chini darini kwa ndani.

Tafuta fundi wa hizo paa za kuficha hakikisha ni mzuri otherwise nazo huwa zinavuja sana kwenye maungio ya bati na zege lililoficha paa ( upstanding walls or gutter)
 
Zege ni ghali zaidi kama unataka kuokoa gharama. Pia zege ukiezekea lazima juu yake uweke material ya water proof vinginevyo likinyonya maji wakati wa mvua nyingi utakuja kukuta linavuja na litakuwekea alama chini darini kwa ndani. Tafuta fundi wa hizo paa za kuficha hakikisha ni mzuri otherwise nazo huwa zinavuja sana kwenye maungio ya bati na zege lililoficha paa ( upstanding walls or gutter)
Asante kwa angalizo la changamoto ya kuvuja.
 
Sisi matajiri ndiyo Nyumba zetu hizo,tatizo akijenga mtu mweusi jiandae kwa presha na kisukari!
25678901.jpg
 
Kaka unapatikana wapi mkuu.
Tuwasiane kwa
0753961896

Nitakwambia jambo
 
Back
Top Bottom