Nyumba ya Maajabu Masaki!

Nyumba ya Maajabu Masaki!

Tuendelee brothers and sisters Good evening!
Baada ya umeme kukatika nyumba nzima, ukimya ulitawala nje na ndani. Mkenya hofu ilimtanda sana ikabidi ashuke chini mdogo mdogo katika lile giza maana aliogopa kuwasha tochi ya simu asije akaonekana location alipo. Wakati akishuka alisikia maji yanatoka huko jikoni, moyo ukazidi kwenda mbio. Ikambidi awashe tochi aende mpaka jikoni alipofika akafunga ile koki kimya kidogo kilitawala ghafla akasikia sauti ya mtoto mdogo akicheka huko sebuleni ikambidi aende kucheki na huko kunanini ile amefika tuu umeme nao ukarudi.
Akatoka nje ila hakukuta mbwa hata mmoja na zile damu zote zimefutika, aliozifuta hamjui na huyo mbwa mwingine ameenda wapi pia ikabaki sintofahamu. Ikabidi arudi mbio mbio kwanza kuicheki familia yake kama ipo salama ila cha ajabu alipofika hakumkuta hata mmoja ikabidi aanze kuwaita huku akipita vyumbani kukagua na kujua wameenda wapi. Baada ya kutafuta bila mafanikio huku simu zao zikiwepo hapo ikambidi aende control room ambako ndiko system ya camera zilipo yaani ukitaka kuangalia matukio ya hiyo nyumba inabidi uingie hicho chumba. Hivyo akajaribu kutazama na kuplay back kuangalia matukio yote ila hakuona kitu si nje wala ndani ila matukio mengine yanaonekana ila ya mbwa kuuwawa na familia kupotea hayaonekani.
Mkenya akaamua kupiga simu polisi muda huo network zimerudi kutoa taarifa na kuomba msaada polisi. Kweli baada ya kama dakika 45 walifika na pia baadhi ya watu wake wa karibu. Polisi walikagua ile nyumba yote nje na ndani huku nao pia wakijaribu kutrace chochote ambacho kinaweza patikana cha kuanzia. Ila kila walipokuwa wakitafuta jitihada zao ziligonga mwamba ndipo wakamshauri asuburi siku mbili huku wakiendelea nao kuangalia njia za utatuzi.
Baadhi ya ndugu na jamaa zake walimshauri aende kwenye maombi au alete mtu wa maombi hapo ili kama kuna nguvu za giza basi zishindwe. Ukumbuke pia mkenya aliwahi tokewa na joka. Hivyo akaona huo ni ushauri mzuri, kesho yake kweli alitambulishwa kwa mtumishi vunja vunja ambaye sifa yake kuu ni kuvunja vunja madhabahu zote za kishetani. Basi mtumishi alifika siku ya kwanza akafanya maombi akaondoka. Siku ya pili nayo vivyo hivyo, siku ya tatu mtumishi aliamua kukesha hapo ili wafanye maombi ya usiku kwani alikuwa ameshaona kuna vitu haviko sawa katika hiyo nyumba.
Usiku ulifika baada ya jua kuzama nyumba ilikuwa imepooza ukimya umetanda na huzuni huku ikisindikizwa na sauti za popo wanaopita kuranda randa huku na huko. Maombi yalifanyika sana huku mtumishi akikemea maroho yote, ghafla umeme ukakatika ikabidi mkenya ashtuke ila mtumishi hakushtuka yeye. Basi wakaendelea katikati ya maombi wakasikia mtoto analia huko nje mtumishi akamwambia twende tukakemee sasa wamejileta kwa vunja vunja, wakiwa wanatoka nje hapo kibarazani kwa juu kuna taa hizi za urembo za kuning'inia basi iliachia au kukatika ikadondoka kichwani kwa mtumishi vunja vunja na kumchoma maeneo ya utosoni. Mkenya alichanganyikiwa zaidi hivo akakimbilia getini kujaribu kutoka nje kabisa ya geti, kwa ile spidi aliyotokanayo hakulifikia geti aliteleza akajigonga kwenye kingo ya ukuta zile zimezunguka ukoka!
Je nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Based on true story!
Hiisasanichaivisavyotevinatokeamkenyabadoamen"gan'ganiahapo
 
Story baada ya kufika sehemu ya 3 imepoteza mvuto ghafla hata kama ni chai
 
Warushiane Risasi masaki polisi wasifike kwa hiyo nyumba hatakama ni kesho yake?Chai hii
 
Hello 👋 brothers n sisters Good afternoon!

Tuanze na huu mkasa hapa fuatana nami hadi mwisho. Kuna nyumba hapa Masaki location x, ni ghorofa ya floor moja tuu ndani ina swimming pool, car parking, ina mifumo ya cctv na iko fully furnished. Mmiliki wa hii nyumba ni marehemu Deborah mwenyeji wa maganzo, kishapu mkoani Shinyanga.

Deborah alikuwa ameolewa na alibahatika kupata watoto watatu wote wa kiume na mumewe alikuwa mfanyabiashara wa madini huko Kahama na Katoro. Kutokana na ukwasi aliokuwa nao mumewe waliamua kununua nyumba Dar es Salaam hapa Masaki kwa bei ambayo haikuwekwa wazi. Mume wa Deborah aliamua kuihamishia familia yake yote hapo ili iwe maskani yao rasmi.

Baada ya kuingia kwenye hiyo nyumba, wivu ulitaradadi sana kutoka kwa ndugu upande wa mume na hivyo njama zikasukwa za kumpoteza mume na mke ili ndugu warithi zile mali; jitihada zilifanyika na msimu wa majira ya masika, wakina Deborah walivamiwa nyumbani kwao na kuuawa na majambazi baada ya majibizano ya hapa na pale ya kurushiana risasi. Baada ya mume kuuawa kwa kupigwa risasi, Deborah alichinjwa na wale majambazi yeye na wanawe wote watatu. Kisha ikachukuliwa hydrofluoric acid na kutumika kuyeyusha miili hiyo ndani ya shimo kubwa lililo chimbwa huko ndani. Baada ya hapo pakafukiwa vizuri na wakachinjwa mbuzi wawili hapo hapo.

Kutokana na ukimya wa haya maeneo na kila mtu kujali ya kwake, ikapita muda mrefu kidogo haswa ukizingatia alikuwa ni mtu wa masafa sana katika kufanya biashara hiyo madini. Basi ndugu waliingia na wasiwasi ikabidi kwenda kumtembelea na wakabisha hodi bila mafanikio na simu zake zilikuwa hazipatikani. Ila taa zilikuwa usiku zinawaka na alfajiri zinazima( photosensors device). Na kwa sababu ya ushua wa hayo maeneo hakuna mtu alikuwa ana taarifa zake, hivyo ikabidi waende kwa mwenyekiti kisha polisi. Ikaamuliwa waingie ndani kwa kuvunja geti dogo ambapo walifanikiwa. Wakaingia ndani vitu vilikuwepo ila wao hawapo na walipoingia ndani simu zipo ila wao hawapo. Wauaji utaalamu mzuri sana wakutokuacha ushahidi wowote. Hivyo nyumba ilikaa chini ya uchunguzi na upelelezi mpaka pale polisi ilipoamua kuirejesha kwa familia.

Familia ilikaa kila mtu akiwa na majonzi na maswali kichwani za pande zote mbili. Ukaja katika upande wa usimamizi wa mali maana hakukuwa na mgawanyo maana haijajulikana wako hai au wamekufa? Hivyo ikaamuliwa upande wa mume yaani kaka mtu atasimamia mali za nduguye.

Kaka mtu alienda kuishi pale masaki kwa muda wa miezi 6 huku akifanya ufuatiliaji polisi wa upotevu wa mdogo wake na familia yake kusikojulikana. Baada ya hio miezi sita akaamua aipangishe hiyo nyumba sasa ili ilete kipato zaidi. Mpangaji wa kwanza kuingia pale alikuwa ni wakutoka Kenya ambaye alikuwa akifanya kazi katika taasisi x ya kifedha hapa nchini kama manager.

Alihamia yeye na wanaye wawili, mke wake, dada wakazi na mtoto wa dada yake. Maisha yalikuwa mazuri na yakawaida yenye ubusy na upweke haswa ukizingatia kila yupo na mambo yake. Weekend moja walipanga wote kutoka out kwenda beach kuinjoy hivyo nyumbani alibaki dada wa kazi mwenyewe. Akiwa ameketi kwenye sofa sebuleni amejiachia zake akasikia sufuria imedondoka jikoni, hakujali akaendelea kuangalia tv ghafla tena akasikia mlango wa kabati jikoni kama umefunguliwa, ikabidi apunguze sauti ya TV ili asikilizie sahii sasa lilianguka beseni chini moyo wake ukaanza kwenda mbio ikabidi asogee taratibu uelekeo wa jikoni kutazama nini kinaendelea huko. Alipokaribia akasikia kitu kimetua chini kwa kishindo puu! Akajikuta amepiga yowe tuu, na paka naye akampitia miguuni akilia. Akashusha pumzi kidogo maana alishatepeta, walikuwa wana paka hapo kwao na mbwa pia alikuwepo ila kwa hapo jikoni ni paka alikuwa akitafuta vitafunwa tu. Hivyo alirudi sebuleni kukaa na paka naye akaja kukaa pembeni yake. Alijihisi kuchoka hivyo usingizi ukampitia, akaja kuamshwa na kelele za paka huko store. Ikabidi aende ila wakati anaenda akasikia kimya ghafla akahisi au amedaka panya. Alipoanza kukaribia akaona matone ya damu, aliposhupaza shingo kuangalia huko store paka alikuwa ameshakufa. Alipigwa na butwaa sana akawaza nini kimemua huyu paka?

Twende kwa bwana mkenya sasa, alipokuwa akirudi ametokea beach na familia njiani maeneo ya chole aligonga gari aina ya prado ubavuni huku kwenye taa. Kwa hofu hakusimama akaamua kukanyaga mafuta na kuondoka. Akafika nyumbani akiwa amechoka hivyo aliamua kujipumzimsha sebuleni ajipoze na maji baridi kwanza, ndipo anapata taarifa za kifo cha paka wao na yeye anakiri hii siku ilikuwa na mikosi sana. Usiku unaingia kila mtu anaenda kulala na yeye anatoka nje kuwafungulia mbwa.

Akiwa anarudi sasa ili apande ngazi ghorofani akalale ndipo chumba chake kilipokuwepo akakutana na joka kubwa sana jamii ya chatu limeraruka kuanzia hapa mdomoni, kwenye jicho na ubavuni kidogo linatoa damu. Ikabidi asite na afikiche macho ili ajue ni kweli au ni wenge ndipo akasikia sauti ya lile joka likimwambia unaona ulichonifanya leo jioni maeneo ya chole? Mkenya moyo ulipiga pigo moja kubwa kisha akazimia hapo hapo!

Je? Nini kitafata usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua ambao uko based na true story iliyotokea kipindi cha nyuma kidogo.
Peleka Facebook.
 
Story ina tatizo.
1. Ndugu walifanya njama . Sasa inakuwaje tena wanakuwa hawajui?
2. Majibizano ya risasi. Halafu nyumba iwe kimya ushuani. Kwanini polisi hawakuja kufuatilia kilichotikea na majirani?
3.
 
Back
Top Bottom