warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Mambo ya Urithi! Moja ya nyumba mbili zilizoachwa na marehemu Muhidin Maalim ‘Gurumo' iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, ambayo ndiyo anayoishi mkewe Pili Saidi, ipo sokoni baada ya watoto wake kung' ang' ania iuzwe.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika watoto hao wapatao sita , wamemlazimisha mama yao huyo wa kambo kukubaliana nao kuhusu jambo hilo, wakiahidi kumpatia fungu lake, kwani wao wanataka kugawana mali iliyochumwa na baba yao.
"Yule mama yupo kwenye kipindi kigumu kweli , maana wale watoto hawana ushirikiano naye kabisa , sijui ataishi kwenye mazingira gani na sidhani kama wanampa msaada wowote wa kujikimu kimaisha" kilisema chanzo chetu.
Bi Pili alipoulizwa juu ya ukweli wa habari hizo, alikiri nyumba kuwa njiani kuuzwa kwani yeye hana uwezo wa kupingana na watoto wa marehemu, hivyo amekubaliana nao ili kujiepusha na mabalaa mengine.
"Ni kweli hii nyumba watoto wa marehemu wote wamekubaliana kuiuza ili wagawane na wameahidi kunipa fungu langu, siwezi kupingana na hilo kwa kuwa mimi sikubahatika kumzalia, japo sijui hatma ya maisha yangu nitakapoondoka humu ndani maana hawa vijana hatuna ushirikiano mzuri kwa sasa''.
Alisema hata gari ya marehemu aliyozawadiwa na Diamond ilitaka kuuzwa lakini akasimama kidete kuitetea kwa kuwa msanii huyo alimwambia kwa kuwa mumewe amefariki basi itakuwa mali yake na kusema inamsaidia kujikimu kimaisha kwani anaifanyia biashara.