Nyumba ya marehemu Gurumo "for sale"

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mambo ya Urithi! Moja ya nyumba mbili zilizoachwa na marehemu Muhidin Maalim ‘Gurumo' iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, ambayo ndiyo anayoishi mkewe Pili Saidi, ipo sokoni baada ya watoto wake kung' ang' ania iuzwe.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika watoto hao wapatao sita , wamemlazimisha mama yao huyo wa kambo kukubaliana nao kuhusu jambo hilo, wakiahidi kumpatia fungu lake, kwani wao wanataka kugawana mali iliyochumwa na baba yao.

"Yule mama yupo kwenye kipindi kigumu kweli , maana wale watoto hawana ushirikiano naye kabisa , sijui ataishi kwenye mazingira gani na sidhani kama wanampa msaada wowote wa kujikimu kimaisha" kilisema chanzo chetu.

Bi Pili alipoulizwa juu ya ukweli wa habari hizo, alikiri nyumba kuwa njiani kuuzwa kwani yeye hana uwezo wa kupingana na watoto wa marehemu, hivyo amekubaliana nao ili kujiepusha na mabalaa mengine.

"Ni kweli hii nyumba watoto wa marehemu wote wamekubaliana kuiuza ili wagawane na wameahidi kunipa fungu langu, siwezi kupingana na hilo kwa kuwa mimi sikubahatika kumzalia, japo sijui hatma ya maisha yangu nitakapoondoka humu ndani maana hawa vijana hatuna ushirikiano mzuri kwa sasa''.

Alisema hata gari ya marehemu aliyozawadiwa na Diamond ilitaka kuuzwa lakini akasimama kidete kuitetea kwa kuwa msanii huyo alimwambia kwa kuwa mumewe amefariki basi itakuwa mali yake na kusema inamsaidia kujikimu kimaisha kwani anaifanyia biashara.
 

Attachments

  • 1415203788144.jpg
    44 KB · Views: 2,329
Mwenyewe aliimba lakini, hao watoto nao ni nuksi
 
Ndio tatizo la hawa watoto wanaoona cha baba ni chao,badala ya kuhangaika kutafuta vya kwao wanakimbilia kurithii tu..ukiwa na watoto dizaini hii watakuwa wanakuombea ufe mapema wagawane mali zako..dawa nikuandika wosia tu nikifa mali zangu ziende kwa Yatima ukapate thawabu uko Mbinguni
 

Hahahaaaaa
 

yaani ktk maisha ndugu zangu jf tujitahidi sana turithishe watoto wetu elimu
elimu ndo kila kitu
 
Acha wauze ili wajifunze pesa ni makaratasi........mbaya zaidi zikishateketea ndio basi tena watabaki kusimulia hadi vitukuu umaarufu wa baba yao .......hapo bendi ya Msondo italaumiwa kwa "kuwatupa watoto wa mzee Ngurumo" .......
 
waache wauze wàkatese bar
cpat pic km mzee wao añgekuwa kajiwekeza
mbna wangeuanà lol!!!
 
Acha wauze ili wajifunze pesa ni makaratasi........mbaya zaidi zikishateketea ndio basi tena watabaki kusimulia hadi vitukuu umaarufu wa baba yao .......hapo bendi ya Msondo italaumiwa kwa "kuwatupa watoto wa mzee Ngurumo" .......

Hizo hela zikishapatikana na undugu wao unaisha hapo hapo,nadhani waliouza nyumba za urithi wana uzoefu na hilo.
 

Bonge la sefu kontena,waache watoane roho kwa mali alizoaacha baba yao!
 
Ndo shida ya kuwalea watoto kimasikini. Baada ya mzee kufa wanaanza kugombania kila kitu hadi nguo.
 
Tatizo alilitaka mwenyewe marehemu mzee Gurumo hakuwaandaa kujitegemea ndio maana mali ya babayao inawatoa roho.
"Tunatoana roho yarabiii iii,,, kwa mali aliyoacha baba ahaaaaa"x2 Ngurumo alikuwa genius sema siifahamu vizuri hii nyimbo... hebu ongeza mistari mingine kama unaifahamu!
 

ushauri mzuri huu......unajitahidi kuwapa msingi mzuri wa elimu basi.......wakizembea inakula kwao na mali hawapati......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…