Nyumba ya muigizaji wa filamu, Batuli imetekea kwa moto. Nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
Nilikuwa saluni najiandaa ili niende kwenye fainali za TMT ndipo nilipopigiwa simu na majirani majira ya saa tatu usiku kuwa nyumba yangu inaungua na imeteketea yote kwa moto, Batuli aliiambia Clouds FM.
Iliniuma sana vitu vilivyonusurika ni magari yangu tu mawili, alisema kwa uchungu.
Aliongeza kuwa majirani walihisi chanzo cha moto huo kinaweza kuwa ni umeme. Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa.