Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Chizzo,Chizzo,
Nilisoma Nyaraka za Bilal Rehani Waikela katika Maktaba ya Muslim Student Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) miaka ya 1980s nikiwa mwanafunzi hapo chuoni na pia Katibu wa MSAUD.
Hizi nyaraka zilitakiwa zote zichomwe moto baada ya kumalizika mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na kuundwa BAKWATA.
Hii ilikuwa amri kutoka juu alivyonieleza Mzee Waikela.
Mzee Waikela yeye alikuwa katika Tume ya Mussa Kwikima iliyoundwa kutafuta suluhu ya mgogoro ule.
Mzee Waikela alizificha nyaraka zake zote pamoja na cutting za magazeti kwa miaka 20 kisha akazileta MSAUD kwa matunzo ili Waislam wajue ukweli wa mgogoro ule.
Wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes nilisafiri hadi Tabora na nikafanya mahojiano na yeye nyumbani kwake pamoja na wazalendo wengine na wote wametangulia mbele ya haki kuhusu mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Waikela akanieleza mambo mengi yaliyotokea hasa baada ya uhuru mwaka wa 1961 hadi kufikia mwaka wa 1968 EAMWS ilipovunjwa na serikali.
Waikela anasema sababu ilikuwa EAMWS chini ya uongozi wa Aga Khan, Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir ilikuwa inajenga Chuo Kikuu na serikali haikupendezewa na jambo hili.
Historia hii ipo katika sehemu ya tatu na ya mwisho katika kitabu cha Abdul Sykes kilichochapwa London mwaka wa 1998.
Nakukamilishia picha yako.