Nyumba yenye thamani ya milioni 45

GOSSO MZEKEZEKE

Senior Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
180
Reaction score
204
Habari zenu wana JF

Kuna nyumba inauzwa milioni 45 maeneo ya Kivule, ina sebule, dinning, jiko, vyumba vitatu vya kulala na kimoja master. tiles kote, madirisha ya aluminium, gril, matanki ya vyoo, maji ndani na umeme upo tayari, n.k. Nataka niendek benki nichukue mkopo nikanunue, je napigwa au ni sawa tu. inahitaji service kidogo tu. Naombeni ushauri
 
Kununua nyumba ni jambo jema ila ni jambo hatari sana maana watanzania ni wapigaji.

Kuna watu wanaitwa jenga uza.. huwa wanajenga nyumba ya quality ya chini kisha anaifanyia finishing kalii ya rangii na gypsum ili ivutie na kupendeza machoni kumbe tofali zake ni michanga tupu. Kisha wanatafuta mteja wanamuuzia kwa bei yenye faida kubwa kwao

Kama una uwezo wa kukopa milion 45 na unahitaji nyumba ya kuishi. Nakushauri kopa hela na ujenge mwenyewe.

Kivule viwanja vizuri vya milioni 5 vipo kibao.

Nunua kiwanja cha milioni 5. Kisha milioni 40 jenga nyumba mwenyewe ukisimamia. Uone utavyopata kitu kizuri
 
Asante kwa ushauri mzuri.
 
Wilaya ya Ilala DSM. Unapita banana then kitunda then unaenda au fremu kumi na huko ndio kivule.
ukinunua hiyo nyumba sasa kwa 45mil, baada ya miaka mitano ukitaka kuiuza thamani yake itakuwaje?

Mwaka fulani, miaka kama mitano hivi iliyopita, jamaa yangu mmoja alikopa bank na akabond nyumba yake. Alithamanisha nyumba yake kwa 100mil. Valuer wa benki alipokwenda mbagala kiburugwa kuiona nyumba akaivalue kwa 40mil. Akamwambia ingekuwa eneo lolote la wilaya ya kinondoni angeivalue kwa 150mil.

My Point; Uthamani wa nyumba unategemea eneo ilipo. kuwa mwangalifu
 
Akupe picha za mchakato wa ujenzi uone ni ubora gani ulitumika, angalau inaweza sema kitu ingawa sio definitive
 
Asante kwa maoni.
 
Uyu jamaa kamaliza yote. Jenga nyumba yako mwenyewe kwa quality unayoitaka wewe. Full stop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…