Uchaguzi 2020 Nyumba za ibada zapigwa marufuku kufanyia kampeni za wagombea

Uchaguzi 2020 Nyumba za ibada zapigwa marufuku kufanyia kampeni za wagombea

Kamati ya amani nchini inayoongozwa na Mwenyekiti wake na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa, imepiga marufuku makanisa na misikiti, kutumika kumfanyia kampeni mgombea yoyote wa chama cha siasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki waumini wake.

Wametoa agizo hilo leo Septemba 26, 2020, jijini Dar es salaam, wakati wakizungumza na wandishi wa habari ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sheikh Alhadi Mussa Salum, amesema kwa kufanya hivyo inawezekana ikawa chanzo cha kuvuruga amani ya nchi.

"Muacheni mtu akamchague kiongozi anayemtaka na sio wewe kiongozi wa dini fulani unatumia nyumba za ibada kama ni jukwaa la kisiasa"amesema mwenyekiti wa kamati hiyo Shekh Alhad Musa Salum.

Kushoto ni Mjumbe wa kamati ya amani nchini Sylvester Gamanywa, katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh Alhad Mussa na kulia ni Makamu Mwenyekiti George Fupe.

Amesema kama kila kiongozi wa dini ataamua kufanya hivyo amani ya nchi tunaweza kuivuruga hivyo amewataka viongozi dini kushirikiana katika kupinga kutumia nyumba za ibada kunadi sera zao.
Mbona mwamakula na katimba sasa badala ya sara amekuwa mtoa sera wa chadema ila watu wamekaa kimya?
Ila akisemea kwenye kanisa tutampigia kerere.
 
Si vyema kwa lugha uliyotumia, hata Sauli a.k.a Paulo alikuwa muuaji lakini akaongoka.Usihukumu ukaja ukumiwa.Mwombe radhi shehe.
Shekhe shehena! Huyo mshirikina tu! Hivi ile dua yake aliyomuombea Mange Kimambi na akatangaza kabisa huwa Mange hamalizi mwaka vipi alifanikiwa au?!
Kauli yake ile ndio iliyonifanya nizidi kumuweka kwenye kundi la washirikina tu!!
 
Si vyema kwa lugha uliyotumia, hata Sauli a.k.a Paulo alikuwa muuaji lakini akaongoka.Usihukumu ukaja ukumiwa.Mwombe radhi shehe.
Then kuna jamaa ninaemfahamu pia aliwahi kupeleka kesi yake yeye na mkewe kuhusu swala la talaka kwa huyo shekhe wako akashauri jamaa amuache mkewe, baada ya muda huyo shekhe wako kajimilikisha aliyekuwa mke wa jamaa, sasa wewe unahisi ushekhe gani huo. Shekhe kama shekhe huwa hashauri utoaji wa talaka.
 
Kwa asiyemjua Alhad Mussa alikuwa ni mvuta bangi mzuri tu maeneo ya Makadara. Bwawani hotel disco alikuwa havundi.
Binafsi nashangaa eti Dar Es salaam anaitwa shekhe!?
hana tofauti na Afande Sele mwenye kibali cha kupuliza sigara kubwa hapo PEPONI-MOROGORO, kuna watu wana vibali vya kuvuta kabisa, Sele , Ndatama na Swebe.
 
hana tofauti na Afande Sele mwenye kibali cha kupuliza sigara kubwa hapo PEPONI-MOROGORO, kuna watu wana vibali vya kuvuta kabisa, Sele , Ndatama na Swebe.
Siku niliposkia Alhad Mussa eti ndio shekhe mkuu wa mkoa wa Dar nilicheka sana [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Hii inayojiita kamati ya amani ni uozo mtupu. Kwenye makanisa, kwenye makongamano ya kidini sisiem wanafanya kampeni bila hofu yoyote, hawajawahi kukemewa hawa. Wapinzani hawapewi nafasi hiyo.

Radio Safina Arusha waliandaa kongamano la maombi mwezi wa 9 mwanzoni. Waziri mkuu pamoja na viongozi wa sisiem Arusha pamoja na mgombea ubunge wao Mrisho gambo, walivamia kongamano hilo kwa gia kwamba wamealikwa, wakatumia mwanya huo kufanya kampeni wazi wazi bila kujali watu pale walikusanyika kwa ajili ya maombi tu na si kampeni za sisiem. Sikuwahi kuiskia hii kamati ikilaani kitendo hiki kiovu.

Binafsi nilikwazika sana kwani nilijiandaa kwa maombi tu na si kusikia kampeni za sisiem kwenye kongamano hili. Bora Radio Safina wangetutangazia mapema ili tusishiriki uchafu huu. Imagine baada ya kufanya kampeni zao waliondoka, wangekaa basi hadi mwisho tujue kweli walienda kumtafuta Mungu.
 
Back
Top Bottom