Nyumba za kupanga, fremu za kisasa sio dili sasa yani kila mtu kawekeza huko

Nyumba za kupanga, fremu za kisasa sio dili sasa yani kila mtu kawekeza huko

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,749
Reaction score
37,420
Kuna uzi nilisema kuhusu biashara ni mda ,wakati,mapungufu na eneo.

Ila kwa sasa kila kona hakuna cha mkoani wala cha wapi ,kila mtu anatengeneza nyumba za kupangisha za kisasa au fremu zenye mvuto ambazo zina parking na gorofa.

Kama unapesa zako ndio unataka kuwekeza huku nakushauri labda angalia uje kwa stahili gani.Maana mpaka chanika ,morogoro,dodoma na katoro zipo nyingi.
 
Nikufahamishe tu Tanzania ina upungufu wa nyumba milioni 3 na kila mwaka zinajengwa nyumba 200,000 tu. Sasa jiulize huo uhaba utaisha lini na population inaongezeka kila siku.
Msipende kutoa hitimisho kwa kuangalia mtaani kwenu tu.
 
Ni kufahamishe tu.Kuna watu sasa wanatengeneza hizo nyumba na kodi ni ndogo kama una ka mtaji ka kufikiria unarudisha faida ondoa.Leo kariakoo fremu shingapi hapo na unaweza kumiliki
 
una point kubwa sana.

Na hii imesababishwa na ufisadi uliokisiri.

Wakishaiba mafedha huko na hawana pa kuyaweka nje ya nchi wanajaza majumba.

Real estate is oversaturated.
 
Ni kufahamishe tu.Kuna watu sasa wanatengeneza hizo nyumba na kodi ni ndogo kama una ka mtaji ka kufikiria unarudisha faida ondoa.Leo kariakoo fremu shingapi hapo na unaweza kumiliki
Kodi ndogo labda kijijini kwenu hapa Dar na miji mikubwa yote nyumba za kueleweka kodi ipo juu na zipo chache. Unajua kodi ya nyumba ya vyumba hata viwili Sinza,Kinondoni,Makumbusho,Kijitonyama,Mwenge,Tegeta,Goba? Au unazungumzia kodi za Tamdale?
 
Nikufahamishe tu Tanzania ina upungufu wa nyumba milioni 3 na kila mwaka zinajengwa nyumba 200,000 tu. Sasa jiulize huo uhaba utaisha lini na population inaongezeka kila siku.
Msipende kutoa hitimisho kwa kuangalia mtaani kwenu tu.
Pacha naona una hobi ya kujenga, kuna mahali nipo natamani nikushauri uje uwekeze
 
Frem naweza kukubaliana na wewe, ila nyumba za kupanga hapana.
Wachimba madini,ccm na matapeli wote wamewekeza huko na tena mpaka mangaji anauliza kuna wifi
 
una point kubwa sana.

Na hii imesababishwa na ufisadi uliokisiri.

Wakishaiba mafedha huko na hawana pa kuyaweka nje ya nchi wanajaza majumba.

Real estate is oversaturated.
Mkuu inategemea, kwa sasa, kupanga nyumba nzima au apartment inaweza kugharimu mpaka laki nane kwa mwezi, na watu bado wanataka kodi ya mwaka mzima na zinajaa. Kingine ardhi na eneo vinaenda vinapanda thamani, bora mtu kama anaweza ajenge tu.

Kingine takwimu za kitaalamu zinaonyesha bado tuna upungufu wa makazi, ukienda level ya makazi bora ndi bado tabu ipo. Pia Watu wanaongezeka kwa kasi nchi hii.

Labda unadhani wafanye biashara gani mkuu,huwa natamani sana mtu akielezea kitu anaonyesha na suluhisho au jambo jingine la kufanya. Je upo katika real estate, au umehukumu kwa observation tu.

Jambo jingine watu wanatengeneza mashine ya pesa au tuite system, hilo jengo linatumika kukopea na kufanya mambo mengine kama kuepuka kodi na kuchuma faida ya mifumo ya kikodi.

Sipo katika real estate lakini kuna mambo wanajua wanachofanya hawa watu, sio mapunguani hawa wanaokazana kuyaotesha magorofa na kuyapangisha.

Kuna msemo unasema kopa pesa kidogo bank na utakuwa katika matatizo, kopa pesa nyingi sana benki inakuwa katika matatizo, yani wewe ndio kama unalelewa ili usile loss wakaumia
 
Kuna uzi nilisema kuhusu biashara ni mda ,wakati,mapungufu na eneo.

Ila kwa sasa kila kona hakuna cha mkoani wala cha wapi ,kila mtu anatengeneza nyumba za kupangisha za kisasa au fremu zenye mvuto ambazo zina parking na gorofa.

Kama unapesa zako ndio unataka kuwekeza huku nakushauri labda angalia uje kwa stahili gani.Maana mpaka chanika ,morogoro,dodoma na katoro zipo nyingi.
Sasa unatafuta uwekezaji utakao fanya peke yako .

Au unafanya uwekezaji utakao kuweka salama kiuchumi
 
Back
Top Bottom