Umejuaje mkuu....Santieli hii tabia ya wenye nyumba au wapangaji kumsalimia nakuitikia kwa sauti ya chini ama asiitikie kabisa chakufanya nikuacha kumsalimia kiumbe yeyote ukiamka asubuhi lazima watanyooka tu maana tabia hiyo imekuwa sugu kwenye nyumba nyingi sana
Sent using IPhone X
Wenye nyumba ni wasumbufu baadhi yao au wengi wao......lakini baadhi ya wapangaji nao dah...ni shughuli kwa kweli...Wakuu walahi mtu unaweza tamani upate walau pesa ya shortcut ili uweze kununua au kujenga banda lako mwenyewe ka kujiegesha ili kuepukana na changamoto za nyumba za kupanga....
Mafano mimi nimepanga nyumba moja hivi, gharama yake kwa mwezi sio kubwa ni kawaida. Nikaamua niwe muungwana nikamwambia mama mwenye nyumba, "maji na umeme nitalipa" akafurahi na kuridhia.Nina miaka miwili sasa yeye mara nyingi alikua hashindi nyumbani maana alikua matron shule moja ya mission kwa hiyo kaa yake pale nyumbani ilikua likizo ya mwezi wa sita au 12...
Kodi nalipa miezi mitatu mitatu na sicheleweshi
Hivi karibuni kafukuzwa kazi kutokana na kutokua na mahusiano mazuri na wanafunzi shuleni.... Sasa kimbembe kimemkuta mke wangu pale home..
.1) Mke akiamka akimsalimia mama mwenye nyumba haitiki sikunyingine aitike sauti ya chini....
2) watoto wake wakikaa na mke wangu ananuna hadi kwa watoto wake hata wiki mbili ..
3) Mtoto wangu siku nyingine amtolee mimacho ya kuogofya ili kumtisha mtoto asiingie ndani kwake ila nikiwepo na akajua anajifanya kumpenda na kumuitaita....
4) kumbambikiza chuki mke wangu kwa majirani lakini majirani hawaoni ubaya wake wanakuja kumuambia mke wangu yoyote aliyosema.....
Aisee ni mengi yaani mlio na vibanda au nyumba zenu hongereni, ila sisi wengine ambao bado nadhani tutamaliza nyumba kwa kuhamahama....
Wale wa nyumba za mfukoni kama mimi mnaishije?
Nokia kitochi
Kweli kabisa siku niliyohamia nyumbani kwangu nililala siku tatu mfululizo nakoroma tu....Pambana ujenge yako bro utakuwa na amani sana.
Yaa kunawakati ni ligi....Wenye nyumba ni wasumbufu baadhi yao au wengi wao......lakini baadhi ya wapangaji nao dah...ni shughuli kwa kweli...
Asante mkuu hapa na copy na ku pasteMwambie mke wako asimjali huyo mama mwenye nyumba, na wewe usijali huyo mama mwenye nyumba, watoto wako wasimjali huyo mama mwenye nyumba, wote mkisikia maneno kuhusu nyingi kaeni kimya na msiwe na mpango wa kujua kasema nini. Believe me, mwezi mmoja mwingi atapata akili
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna moja hiyo rafiki yangu, alikuwa anatoa mtoto mdogo nje (40) sasa akawa ameita shehe ili mtoto asomewe dua baada ya kunyolewa nywele. Aisee mama mwenye nyumba eti mlokole akakataa hataki mambo hayo. Rafiki yangu aliponipigia nikamwambia niachie mimi hiyo, wewe andaa chai, maandazi, chapati, roast maini na mkeka. Mambo ya shehe na ubani niachie mimi, muda ulipofika tukaingia na watu 3 wote tumekula suti kaliii, na kibegi chetu. Tukaingia ndani shehe kavua koti kapiga kanzu, tukaanza kupiga dua freshi, mtoto akanyolewa safi, dua ikaendelea, then tukagonga roast na chapati safiii. Na mama mlokole naye akapelekewa roast maini na chapati akagonga huku akiomba aongezewe...Kinachonikera n mtu kukupangia
Chakula ndan kwako et kitomoto
Marufuku wanakera Hawa wamama
Sent using Jamii Forums mobile app