Nyumba za kupanga na adha zake

Nyumba za kupanga na adha zake

Santieli hii tabia ya wenye nyumba au wapangaji kumsalimia nakuitikia kwa sauti ya chini ama asiitikie kabisa chakufanya nikuacha kumsalimia kiumbe yeyote ukiamka asubuhi lazima watanyooka tu maana tabia hiyo imekuwa sugu kwenye nyumba nyingi sana


Sent using IPhone X
Umejuaje mkuu....
Sa hivi nimemlisha mke wangu ujinga kwamba we ukimuona mpite tu, ili akitafuta kasababu shukanae mzima mzima.....

Nokia kitochi
 
Wakuu walahi mtu unaweza tamani upate walau pesa ya shortcut ili uweze kununua au kujenga banda lako mwenyewe ka kujiegesha ili kuepukana na changamoto za nyumba za kupanga....

Mafano mimi nimepanga nyumba moja hivi, gharama yake kwa mwezi sio kubwa ni kawaida. Nikaamua niwe muungwana nikamwambia mama mwenye nyumba, "maji na umeme nitalipa" akafurahi na kuridhia.Nina miaka miwili sasa yeye mara nyingi alikua hashindi nyumbani maana alikua matron shule moja ya mission kwa hiyo kaa yake pale nyumbani ilikua likizo ya mwezi wa sita au 12...

Kodi nalipa miezi mitatu mitatu na sicheleweshi

Hivi karibuni kafukuzwa kazi kutokana na kutokua na mahusiano mazuri na wanafunzi shuleni.... Sasa kimbembe kimemkuta mke wangu pale home..
.1) Mke akiamka akimsalimia mama mwenye nyumba haitiki sikunyingine aitike sauti ya chini....
2) watoto wake wakikaa na mke wangu ananuna hadi kwa watoto wake hata wiki mbili ..
3) Mtoto wangu siku nyingine amtolee mimacho ya kuogofya ili kumtisha mtoto asiingie ndani kwake ila nikiwepo na akajua anajifanya kumpenda na kumuitaita....

4) kumbambikiza chuki mke wangu kwa majirani lakini majirani hawaoni ubaya wake wanakuja kumuambia mke wangu yoyote aliyosema.....


Aisee ni mengi yaani mlio na vibanda au nyumba zenu hongereni, ila sisi wengine ambao bado nadhani tutamaliza nyumba kwa kuhamahama....

Wale wa nyumba za mfukoni kama mimi mnaishije?

Nokia kitochi
Wenye nyumba ni wasumbufu baadhi yao au wengi wao......lakini baadhi ya wapangaji nao dah...ni shughuli kwa kweli...
 
Wenye nyumba ni wasumbufu baadhi yao au wengi wao......lakini baadhi ya wapangaji nao dah...ni shughuli kwa kweli...
Yaa kunawakati ni ligi....
nakumbuka zamani wakati nakua niliwahi kukaa jirani na Mzee mmoja mwenye nyumba anaitwa Mzee Kazimoto alikuwa msumbufu kweli kwa wapangaji wake...
ikatokea coincidence ya ajabu akahamia mpangaji mmoja anaitwa Kazikubomoa alikuwa msumbufu kweli kulipa kodi......
hivi vichwa vilisumbuana balaa....yani balaa!!!!
mpaka mwenye nyumba alikimbia nyuma manake alikuwa akiishi hapo hapo....
 
Mwambie mke wako asimjali huyo mama mwenye nyumba, na wewe usijali huyo mama mwenye nyumba, watoto wako wasimjali huyo mama mwenye nyumba, wote mkisikia maneno kuhusu nyingi kaeni kimya na msiwe na mpango wa kujua kasema nini. Believe me, mwezi mmoja mwingi atapata akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie mke wako asimjali huyo mama mwenye nyumba, na wewe usijali huyo mama mwenye nyumba, watoto wako wasimjali huyo mama mwenye nyumba, wote mkisikia maneno kuhusu nyingi kaeni kimya na msiwe na mpango wa kujua kasema nini. Believe me, mwezi mmoja mwingi atapata akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu hapa na copy na ku paste

Nokia kitochi
 
Habarini wana ndugu,

Hii thread ipo special kwa ajili ya kushare kwa pamoja vioja vyote ulivyokutana navyo kwenye nyumba ya kupanga.

Naanza mimi: Kuchota maji ni usiku tu zaidi ya hapo hairuhusiwi hiyo ilikuwa Tabata kwenye bonde la Msimbazi

Pia mwanamke inabidi usibadirishe
 
Kinachonikera n mtu kukupangia
Chakula ndan kwako et kitomoto
Marufuku wanakera Hawa wamama

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna moja hiyo rafiki yangu, alikuwa anatoa mtoto mdogo nje (40) sasa akawa ameita shehe ili mtoto asomewe dua baada ya kunyolewa nywele. Aisee mama mwenye nyumba eti mlokole akakataa hataki mambo hayo. Rafiki yangu aliponipigia nikamwambia niachie mimi hiyo, wewe andaa chai, maandazi, chapati, roast maini na mkeka. Mambo ya shehe na ubani niachie mimi, muda ulipofika tukaingia na watu 3 wote tumekula suti kaliii, na kibegi chetu. Tukaingia ndani shehe kavua koti kapiga kanzu, tukaanza kupiga dua freshi, mtoto akanyolewa safi, dua ikaendelea, then tukagonga roast na chapati safiii. Na mama mlokole naye akapelekewa roast maini na chapati akagonga huku akiomba aongezewe...
 
Hivo vikero vidogo sana unaweza ukajishangaa unakaa hapo 10yrs hujajenga, mm nilikuwa napandishiwa kodi kila baada ya 6month. Nikaona isiwe shida nikakurupuka nikajenga fasta na kumuachia pango la 2month baada ya nyongeza ya 3(16month na 2month akabaki nayo)
 
Back
Top Bottom