Nyumba za kupanga nyingine zina riziki nyingine zina nuksi

Nyumba za kupanga nyingine zina riziki nyingine zina nuksi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Unaweza kuishi nyumba ya laki 3 kwa mwezi lakini cha ajabu kila mwezi unapata hela ya kodi kwa wakati na mwenye nyumba hakuwahi hata kukufuatilia sana,,Lakini ukisema kodi kubwa itakushinda ukasema uende nyumba ya 150,000 basi hapo ndipo mambo yanaanza

Hela ya kodi hupati, unaanza kudaiwa, unachenga chenga na mwisho unaona ile nyumba ya laki 3 ilikuwa na baraka kuliko hii ya bei rahisi ukifanya masihara hata ya laki nanusu inakushinda Mwisho unarudi za uswahilini zile ambazo chooni kumeandikwa mwaga maji ukijisaidia..maisha hata yawe magumu vipi achana na washauri kwamba unatakiwa ukae nyumba za kodi ndogo kaka ishi sehemu nzuri utaweza tu kulipa niamini mimi.
 
Kukaa Pazuri, kula vizuri, kuvaa na kuendesha chuma hivi vitu navipa kipaumbele.

Mengine yatafuata.

Unageuka lini huku, au ndio hadi 2027?
 
NakubaLiana na ww Lakin Pia ukikaa Nyumba ya kodi kubwa na akili & nguvu ya kupambana zaidi inaongezekA.. Mwisho kod kubwa au ndogo inatokana na Hali ya uchumi wa Mtu
 
Back
Top Bottom