kinachotokea hapa ni nchi kukosa maono, nnchi kukosa jukwaa, nchi kukosa msemaji, ama unaweza kuhisi nnchi inakwenda hobelahobela.
nasema hayo kwasababu zile nyumba sina takwimu sahihi Mawaziri wangapi wanaishi mule, ila wengi waligoma hasa kwa kisingizio cha ukaribu na kukosa usiri, kama walivyojadili wanajamii wengine mwanzoni. kama tungekua tunamsemaji wataifa kwa maana ya Rais na mamlaka zake zote mawaziri walipaswa kuishi kwenye zile nyumba, kwa maana ya kurahisisha gharama za ulinzi na mambo mengine.
ila kwa mwanannchi wa kawaida kama mimi nafurahi tunavyoishi nao mitaani japo mitaa ya kunduchi ,Mbezi Beach ndio wanaofaidi, kwasababu yanafasi yakupata huduma nyingi muhimu kama Maji na ulinzi kwa maana walipo hao mabwana wa Ikulu lazima ulinzi uimalishwe, lazima maji hayatakatwa hovyo, umeme utakua na nidhamu , basi tu kupata huduma za kila namna.