Nyumba za NHC hapa mjini kwanini Serikali isiweke sheria wakapangishwa Walimu Madaktari na M-nurse

Kwa serikali hii utasubiri sana

Hii serikali ilijiteua yenyewe
 
Itakuwa msaada mdogo kwa wachache sana.

Badala yake waongezewe maslahi yao kwa kuwana mishahara bora,mikopo yenye riba nafuu (au isiyo na riba /sponsored) au wapewe upendeleo maalumu kwa kuwa na maeneo yao maalumu ya kufanya manunuzi bila kodi au tozo yabidhaa wanazohitaji hasa za ujenzi,chakula na matibabu.Watoto wao wapewe unafuu wa ada wanazolipa shuleni na vyuoni.Project ya hivyo lazima iwainue na kuwaheshimisha watu wa kada hizo hizo tajwa.
 
Baada ya miezi michache utasikia huyo muhindi anampa mwalimu mil 10 ili ampishe. Mwalimu nae ana kibanda chake bado kupaua na madirisha, anakubali kuchukua hela. Miaka michache tunarudi kulekule
 
mkuu ni wazo zuri.na pale ambapo nyumba za watumishi hazipo,zijengwe.
Hizo za zamani zivunjwe zijengwe kubwa zaidi za kisasa wakae familia nyingi tena kwa bei nafuu. Tatizo NHC badala wajenge wenyewe, watatafuta mwekezaji eti wagawane Friday, bdae utasikia kodi laki 7. Wataishia kukaa wenye uwezo mkubwa
 
mlaniwe wote mnaotaka kulaniana na manofikilia kulaniana wakati hizi nyumba hazituhusu ni za wahindi kwani walinyanganywa enzi hizooo nyie mmekuja juzi mjini mnazitaka , kajenge zakwenu huko kibamba
Acquisition of Building Act 1971 - nyumba zenye thamani ya shs 100,000+ zilitaifishwa - za wahindi - za waswahili ziliachwa -mfano nyumba ya John Rupia na Chauremo hapo Msimbazi - wakati huo wamiliki wa kihindi wakitoza kodi ya shs 300 leo NHC inatoza 500,000 fleti hiyo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…