Ni kweli kijana tunatakiwa kuleta hela nchini,watu wa Africa magharibi wamejitahidi kutuma dolar nyingi nchinii mwao km zawadi kuwekeza na mengine mengi tofauti na sisi. Nchi km China, Pakistani, Korea,I ndia etc zinakadiriwa kupeleka hela chini mwao km misaada kwa jamaa na ndugu pekee kwa kiasi ambacho hata nchi za magharibu wamefika mahali pa kuangalia kwa makini. Mara nyingine wanachukulia km inawapunguzia mzigo wa kutoa misaada,na mara nyingi wanona kuwa ni threat ktk uchumi wao.
Statistics za makampuni ya money transfer companiies km Western Union zinaonyesha Hela za kutisha zikielekea Asia na kidogo Africa Magharibi. Hapo ndipo tutakapoona ubunifu wa wezetu ktk hii huduma na baadaye kujikita nchi masikini. Hawa jamaa jamaa wanatoa huduma ya kupeleka hela ila pia wanafanya kazi nzuri ya kuzirudisha. Wamejitahidi kujikita nchi masikini na kujenga faida kubwa ambayo mwishowe inawekwa ktk hard currency na kurudishwa.
Said sasa wewe umeweka wazo tunahitaji wataalamu wa uchumi nao waje na ujanja wa kuzipata hizi hela zilizojificha ktk hii reserve.Hapa panahitaji kuona mbali,si tuvutie hela ambayo mwishowa siku tunakuta tulifanyia tumbo.
Nadhani unaona hapo UK walivyoibana hela, ukipiga kazi hapo unapata hela ila mwisho wa siku unajikuta kila kitu kimeingia ktk sector za kiingereza na ziada ya kazi ngumu ndio unabaki nayo. Angalia unavyokuwa forced kutumia huduma zao na kulipa rents. Kile kiasi ulichoongezea nguvu za ziada ndicho kinabaki. Sasa sisi wabongo hatujaweza wabana wageni tunaowapa kazi za hela nyingi waziache hizo hela hapa waondoke na bidhaa au na starehe watakayoilipia hapa. Na hii ni rahisi kufanya kwa kutumia wachumi wetu.
idea ya informal sector inabid ikuzwe.Hata marekani kwa mra ya kwanza small companies na informal sector imeleta mapato yaliyowatisha.