Nyumba za Prefab Tanzania

Game Theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2006
Posts
8,546
Reaction score
855



Kutokana na usanii mwingi uliojaa na cost za kujenga zilivyokubwa nchi hii, nauliza

what are the chances za biashara au kujenga mwenyewe ya pre-fab houses ?

Say unajenga nyumba nzima nje ya nchi kwenye viwanda vya kufanya hivyo kisha wanaleta Tanzania kwa ajili ya assembling ambayo give or take inaweza ikachukua 4 weeks max

je mnaonaje idea hiyo au mazingira hayaruhusu? na kama haya ruhusu je kuna mambo gani ya kuzingatia mfano:

Sheria zinasemaje?

Je nyumba hizi zinaweza kulast up to 80 yrs max au?

costs zinasemaje?

etc

anyone?
 
Ndio naskia leo, teknolojia kweli imenipita.
Vipi kuisafirisha? Ushuru wa kuitoa bandarini, gharama ya kiwanja pa kuwekea hiyo kitu.
Halafu huko unapojenga unajengewa bure au?
Nahisi gharama zitakuwa kubwa zaidi.
 
Nafikiri inawezekana, lakini utafanikiwa zaidi uki-lenga kwenye simple designs kwa watu wenye kipato cha chini/ Kati.
Picha hizo mbili ulizoweka ni gharama sana kutengeneza...kwamfano hiyo ya pili gharama ya kutengeneza tu haitakuwa chini ya Milioni 700 (inaweza kufika hata bilioni moja), hapo huja nunua kiwanja, hujaweka hela ya usafirishaji wala kodi zozote!!

 
Reactions: LAT
ninajua factory moja ipo shanghai china prefab house simple design complete with UPVC windows and doors US$ 65.0 per square meter and a normal design from Turkey US$ 800 per square meter
 
this is a good technology na nadhani inawezekana... tatizo ni namna ya kuanza na preservation ya hizo nyumba kutokana na mazingira ya kwetu

Actually kimtindo ni kama tunajenga hivyo tu, maana unakuta mtu anaenda turkey au china analeta kuanzia sementi, misumari, roof hadi vitasa
 

Mkuu Hiyo hapo juu kuna jamaa mmoja amejenga Kinshasa na kaniambia imeoka Germany yaani kila kitu ndani nilimuuliza bei lakini hakuwa tayari kuniambia.

Lakini inafanana na picha hapo juu...Tatizo la Afrika wau wanaogopa mchwa lakini nadhani mbao ni treated.
 
Kweli ni kampuni ya kijerumani (http://www.huf-haus.com/en/home.html)...nilishawahi kuulizia nilipokua Uingereza (wana branch huko), na bei niliyopewa kwa simple design...nyumba ya vyumba viwili vya kulala...single story..waliniambia GBP 200,000/= sawa na TZS 500 milioni! kwa hiyo hapo juu itakuwa ghali sana...,angalia hii site ya UK itakupa picha..... Huf Haus Owners Group - property for sale



 
Ndio Mkuu.. hiyo ya $65 per square meter inafaa kwa hapa TZ!...

ninajua factory moja ipo shanghai china prefab house simple design complete with UPVC windows and doors US$ 65.0 per square meter and a normal design from Turkey US$ 800 per square meter
 

Mkuu hizo ndiyo nyumba zinatumika karibu migodi yote Tanzania, hivyo wasiwasi wako uko tested and so far no drama. Na kama ni mazingira basi ulaya ni midlle east ndiyo hatari zaidi.
 
Kwa wale walio hudhuria Maonyesho ya Kilimo 88 pale Dodoma, kuna kampuni moja ya prefab houses imeishaingia nchini, ofisi zake ziko pale Milenium Bussiness Park. Wamejenga nyumba za mfano pale Nzuguni.

Kwa dar es Salaam, pale eneo la Makumbusho kuna duka la Prefab houses na sample zake pale nje ya ofisi hizo.

Tatizo: Nlipofuatilia cost ya kujenga hizi prefab za Milenium Business Park, cost ya kujenga a small house ya 3 bedroom, one master, jiko, sitting na dinning, ilifika M.78. Kwa M.30, unajenga nyumba nzuri tuu matofali ya playform ukujenga mwenyewe, ukiwacontract NHMBRA (Mwenge) itakicost m.40 tuu.
 
Wapendwa,

Naomba msaada wenu wa kujua nyumba ya namna hii Arusha inaweza kugharimu shilingi ngapi? Nina kiwanja nimenunua maeneo ya USA River/Momela 50mx40m na ninatamani kuanzia mwezi wa saba nianze ujenzi ya nyumba ya makazi.

Chini nataka iwe na three bed rooms, sitting room, dining room, toilet, bathing room, kitchen na store kisha juu iwe na Master bed room na chumba kingine cha watoto. Muenekano wa jengo kwa nje nataka iwe kama inavyoonekana hapa chini.

Lingine ninalotaka kujua ni kuwa kwenye viwanja hivi vya kununua kwa watu ambavyo havijapimwa je ni lazima kuwa construction permit au nikitafuta watu waliosoma Civil Engineering nikawapa ramani hii watanisaidia kujenga bila kuhitaji approval yoyote ya serkali?

 
Hizi zinafaa sana ila hakikisha materials ziko treated well ili mchwa wasizile
 
Hizi zinafaa sana ila hakikisha materials ziko treated well ili mchwa wasizile

mkuu... you could be right ...but most of Prefab houses use steel sections as structures and sandwich panels of steel and UPVC as walls

hivyo hakuna doubt au worry yeyote ile kuhusu mchwa
 
Hivi ile kampuni ya MOLADI imeishia wapi?

nilifkiri wangepata tenda Dar nzima kujenga au?
 


mkuu
hapo katika red nipatie full address zao za ofisi
mf,mobile,landline,fax,email nk
ntashukuru sana
 
TEKNOLOJIA ya prefab haiwezi kuwa na mana kama nayo pia itakuwa ni kitu cha kuagizwa toka nchi za nje. Kimtazamo kwa sababu huko nje vifaa vyote vya ujenzi ni nafuu na vinapatikana, prefab ni kitu cha anasa na hivyo bei yake haishikiki.
SISI Afrika tufanye juu chini ili tutengeneze prefab technogy yetu wenyewe likiwa jibu kwa masikini wetu na vijanaa wanaoanza maisha kwanza, ambao ndio hawana nyumba na sio matajiri...
ILI NCHI YETU NA WATU WAKE WAENDELEE TUKOME KUZUNGUMZZIA KUAGIZA NA KUNUNUA NA TUANZE KUZUNGUMZIA
KUTENGENEZA NA KUUZA NDANI NA NJE YA NCHI...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…