Nyumba za Walimu 562 Kujengwa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Nyumba za Walimu 562 Kujengwa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri OFISI YA RAIS TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali inatarajia kuenga jumla ya nyumba za walimu 562 zitakazochukuwa familia 1,124.

Katimba ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu akijibu swali la Mhe. Jacqueline Andrew aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za Walimu nchini.

"Serikali inatambua uwepo wa changamoto ya upungufu wa nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari nchini ambayo inatakiwa kutatuliwa na Katika mwaka wa fedha 2022/23 na 2023/24, Serikali kupitia fedha za programu za kuimarisha elimu ya Awali na Msingi (BOOST) na Sekondari (SEQUIP) pamoja na fedha za Serikali Kuu, imejenga nyumba 860 za walimu wa shule za msingi na sekondari zitakazochukua familia 2,018 na mwaka wa fedha 2024/2025 serikali itajenga jumla ya nyumba za walimu 562 zitakazochukuwa familia 1,124" - Katimba

Zainab Katimba ameongeza kuwa mpaka sasa serikali imepokea maboma 2,470 ya nyumba za walimu na serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuunga mkono jitihada za wananchi hivyo amewaagiza wakurugenzi wa halamashauri wafanye tathimini ya maboma hayo
GMcDCwJW4AAnyHR.jpg
WhatsApp Image 2024-05-01 at 01.07.16.jpeg
 
Back
Top Bottom