Nyumba za Yamoto: Sheria inahitajika, Fella adaiwa kuwa kikwazo cha Aslay kwenda Wasafi

Nyumba za Yamoto: Sheria inahitajika, Fella adaiwa kuwa kikwazo cha Aslay kwenda Wasafi

chipa GM

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2012
Posts
1,815
Reaction score
2,973
Baada ya kundi la yamoto band kusambaratika kutokana na madogo kutumika kwa mkubwa fela p na Temba bila kufaidi jasho lao hata zile nyumba walizojengewa mkubwa fela kukataa kuwapa.

chanzo cha kuondoka ilikuwa ni zile nyumba ambazo fela alidai kawajengea wale vijana. Mwanzoni mwa mwaka jana madogo walikuwa wanataka wapewe nyumba zao kila mtu afanye mwenyewe finishing.

Mkubwa fela alikuwa mbogo.. hataki kusikia kuhusu nyumba. inasemekana Aslay na BEKA ndiyo walikuwa wakikomalia wapewe nyumba zao.. Kumbe hati za nyumba zote zimeandikwa jina la Diwani wetu wa chama dume. Ina maana siyo za madogo..

Chambuso ndiyo aliwatonya madogo.. Madogo baada ya kuona wanadhulumiwa wakaanzisha mgomo baridi.. Mkubwa Fella akawapa kisogo akaendelea na watoto wengine. Madogo wakajitoa Yamoto.. Mkubwa Fella akafurahi akaona kelele za nyumba zimeshaisha.

Aslay aliwasiliana na Diamond. Kipind Dai yupo South na walikubaliana yeye na Mbosso wataenda Wasafi.. Mkubwa Fella alivyosikia hivyo akamwambia Dai unafeli mwana achana na huyo Dogo. Dogo ana kimeo ana dharau sana. Tumchukue Mbosso tu.. Aslay achana naye.

Nasikia Mkubwa Fella anatafuta mteja wa kuziuza hizo nyumba ili awazime kabsa madogo na huu mpango unasukwa karibu kabisa na Temba. Msando kesi hizi zako mzee!

Diamond umeliacha jembe la kukuingizia pesa kisa huyu Meneja uchwara!?

Hivi watalamu wa sheria hawa madogo hawawezi wakapata haki yao kweli? Hata kwa ushahidi wa kimatukio? Kwa maana hati za nyumba siyo majina yao but kwenye sheria kuna ushahid wa kimazingira.. Nimesahau sikusoma sheria.. Kama kuna mdau anajua sheria fresh aje inbox tuiweke mkakati vizuri.. Haiwezekani madogo waishi kimaskini wakati jasho lao anakula Fella.

Diamond mchukue dogo Aslay.. Fuata ushauri aliokushauri SK.

Mkubwa Fella, rudisha nyumba za madogo wa Ya Moto.. Unajisikiaje watoto wale wamepanga hata Vits hawana?
 
hizi we jamaa huwa hulali
Atalalaje ikiwa alizoea kwenda kwenye ule mtaa wetu pendwa temeke Sudan na tandika sokoni ....vijana wa JUMA pondamali wamekaba mpaka penati ....wamewasepesha na Huduma hamna
Kiufupi wasanii hasa wanamziki wanapunwa sana na hawa ma manager uchwala kama stupid Mkubwa fela...yeye kawafanya mashamba yake ananiudhi.
 
aslay ana kipaji zaidi ya diamond.yule dogo namshauri ruge amchukue . akienda wasafi kipaji chake kitazimwa maana hakuna anaemfikia pale.yule dogo ni brand yeye mwenyewe anaitaji promo tu ya kutosha wasafi sio hadhi yake.aslay ni zaidi ya wasafi
 
aslay ana kipaji zaidi ya diamond.yule dogo namshauri ruge amchukue . akienda wasafi kipaji chake kitazimwa maana hakuna anaemfikia pale.yule dogo ni brand yeye mwenyewe anaitaji promo tu ya kutosha wasafi sio hadhi yake.aslay ni zaidi ya wasafi

True dat.Kipaji chake ni kikubwa sana,akienda Wasafi watamfanyia hujuma na yatakuwa yale yale ya Fella.
 
Mkubwa Fella born town a.k.a mzee wa ndumba akupe nyumba kirahisirahisi tu?[emoji3][emoji3][emoji3]
Kuhusu Aslay kuhamia WCB kwa sasa simshauri, kama kuhamia ingekuwa sahihi kipindi hana hit zake. Kwasasa yuko on fire aendelee kusimama yeye kama yeye
 
Hakuna mdau wa mziki ambae simpendi kama Mkumbwa Fella...jamaa ni mwizi wa haki za wasanii.Anadhani Bongo Fleva ni yake.Juzi juzi hapa Beka Flavour alisema waliondoka Ya Moto wakiwa hawana kitu.Pesa yao yote eti ilitumika kujenga jamaa alkua anawapa tu "pocket money".Imagine hustle ya madogo af eti na nyumba zenyewe wamenyanganywa...duhh.Huyu mtu tumpeleke kwa Mange Kimambi
 
aslay ana kipaji zaidi ya diamond.yule dogo namshauri ruge amchukue . akienda wasafi kipaji chake kitazimwa maana hakuna anaemfikia pale.yule dogo ni brand yeye mwenyewe anaitaji promo tu ya kutosha wasafi sio hadhi yake.aslay ni zaidi ya wasafi
Watu wengine bana....anyway kila mtu na UBONGO asee maadamu smartphone hatujazi wino tunaandika tu
 
Back
Top Bottom