Nyumbani kwenu kuna kitu kilichokuzidi umri au kimeendana umri na wewe!?

Nyumbani kwenu kuna kitu kilichokuzidi umri au kimeendana umri na wewe!?

Msumb

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2022
Posts
3,452
Reaction score
5,372
Habari za mwaka mpya 2024 wapendwa katika Bwana, natumaini wooooote wazima, mwenye changamoto yoyote basi MWENYEZI MUNGU ASAIDIE

Unajua katika majumba yetu tulikozaliwa kuna vitu utavikuta iwe tv, nguo, kabati, meza chochote kile cha zamani kimetunzwa kweli, na bado kinatumika, ukiulizia hiko kitu utaambiwa labda wakati bibi yako mzaa mama anaolewa alipewa zawadi 🤣🤣 dah! Kwaiyo kimekuzidi umri hapo miaka mingi sana

Na kuna kile kitu umezaliwa umekuwa ndo kinaletwa home kwa hiyo hapo ndo kusema mnalingana nacho maana umekiona kimeletwa

Basi mimi kuna mwembe huo Nyumbani ndo nalingana nao umri 😁 maana umepandwa naucheck tu mpaka leo limekuwa likubwa linatoa maembe na limenipita urefu😆

Pia kuna vya kunipita umri miaka na miaka na ni vidogo tu asee, kama vikombe, mikoba mpaka meza inatumika mpaka leo hadi kitanda ase

Ebu tililika na wewe mdau vitu ngani vimekupita umri na vingine mnaringana
 
Kuna Bakuli fulani zipogo kabatini na hazitumikagi niliziona kwenye picha za Harusi ya wazee wangu asee nikashangaa sana
Aisee pale home Kwa madingi Kuna sufuria flani mbili, Moja ndogo na nyingine kubwa saizi ya kati. Ni nzito kweli Sio hizi takataka za siku hizi.

Bi Mkubwa ananiambia Hilo kisufuria kidogo ndicho kilikuwa kinatumika kutupikia uji, kuanzia Kaka yangu wa kwanza mpaka mdogo wetu wa mwisho tangu tumezaliwa, na hiyo sufuria kubwa ndiyo Mzee alikuwa anatumia kupikia enzi za ubachela..
 
Kwa bibi yangu Kuna dishi la bati, anasema watoto wake wote waliogea na bado anaendelea kufulia Hadi leo
 
Nakumbuka ndio nimemaliza form six nimerudi home. Siku Moja baba akanituma nimletee chanuo. Kilikuwa cha mtu. Akaniambia, unajua hiking chanuo kinakuzidi umri? Nilichoka!!
 
Kwa home pale sidhani sana kama Kuna chenye kimenizidi umri......ila Kwa Babu ni hatari "Ogopa"

Kuna jembe la kulimia lile linaevutwa na ng'ombe ni la zamani sana

Kuna planter ya zamani sana

Wheelbarrow kubwa ya zamani sana imeandikwa "ZZK"

Watoto wa 80's njoeni😄
 
Kuna kisu cha kukatia ugali hiki mama alikibebaga wakati ni mfanyakazi wa watu wa mission nimezaliwa nimekikuta na kipo yani bora vyombo vyote viwe vichafu lakini sio hicho kisu
 
ipo Suturia kwa Maelezo ya Marehemu babu ni kwamba alizaliwa 1917 ameikuta. na mpaka sasa inatumika iuchemshia maji ya kuoga, iko kama flying saucer
 
Back
Top Bottom