Nyundo na Wenzake Waomba Mahakama Kufuta Kesi na Hukumu Wakidai Ukiukwaji wa Sheria

Nyundo na Wenzake Waomba Mahakama Kufuta Kesi na Hukumu Wakidai Ukiukwaji wa Sheria

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Dodoma. Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeendelea kusikiliza hoja za rufaa kupinga kifungo cha maisha jela walichohukumiwa Clinton Damas, maarufu Nyundo na wenzake, huku upande wa Jamhuri ukiomba kuzijibu Juni 12, 2025.

Warufani wanaiomba Mahakama kufuta kesi, hati ya mashitaka na hukumu iliyotolewa dhidi yao wakidai ilikuwa kinyume cha sheria.

Waliokata rufaa ni Nyundo aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Amin Lema, Nickson Jackson na aliyekuwa askari Magereza, Praygod Mushi waliotiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Septemba 30, 2024 kwa kosa la kumbaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya, Dar es Salaam.

Pia soma


Akiwasilisha hoja mahakamani hapo leo Jumanne Juni 10, 2025 mbele ya Jaji Amir Mruma, wakili wa warufani hao, Godfrey Wasonga amedai kulikuwa na dosari za kisheria katika kesi hiyo kuanzia hati ya mashitaka hadi hukumu.

Amedai ushahidi wa video uliotolewa mahakamani umeshindwa kuwatia warufani (washtakiwa) hatiani kwa sababu mashitaka waliyoshtakiwa nayo hayakuonekana kwenye video hizo ambayo ni kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume cha maumbile mwathiriwa wa tukio hilo.

Wasonga amedai makosa yanayoonekana kwenye video ni mwathirika wa tukio hilo aliyetambulishwa mahakamani kama XY kuonekana akimnyonya uume mshtakiwa wa pili, kosa ambalo linaangukia kwenye shambulio la aibu ambalo lina vifungu vyake vya sheria.

Kuhusu kurekodi video na kuzitumia mtandaoni, Wasonga amedai kosa hilo linaangukia kwenye Sheria ya Makosa ya Mtandao ambalo lina vifungu vyake vya sheria pia.

Amedai Mahakama ilionyeshwa vipande vinne vya video ambavyo ni 6, 7, 8 na 9 lakini kwenye hukumu vipande vya video vilivyowatia hukumuni ni namba 1, 2, 3 na 4 ambavyo havikuonyeshwa mahakamani hapo.

Kwa mujibu wa wakili huyo, vipande vya video vilivyoonyeshwa viliwaonyesha washtakiwa wakijirekodi wakiwa wanacheza muziki, huku wakiwa na chupa za vinywaji lakini hazikuonyesha wakiwa wanatenda kosa la kubaka kwa kikundi wala kulawiti.

Wasonga amedai maelezo ya shahidi wa tatu ambaye ni mwathirika wa tukio hilo alifika kwenye nyumba baada ya kukubaliana na mtu aliyetajwa kwa jina la Kiboy, ambaye walikutana kimwili na wakati wameshamaliza ndipo watu watano waliingia na kuanza kumbaka na kumwingilia kinyume cha maumbile.

"Sasa hapa tunataka tujue mshtakiwa namba moja alikuwa ni huyu Kiboy ambaye hajatajwa mahali popote hata kuonyeshwa kwenye video, sana sana wanaoonekana ni hawa watuhumiwa wanne ambao wao walikuwa wanacheza na kunywa vinywaji kwenye video hizo," amedai.

Kuhusu video kukutwa kwenye simu ya mrufani wa kwanza ambayo ni aina ya Google Pixel, Wasonga amedai hakuna ushahidi unaoonyesha simu hiyo ilikuwa inamilikiwa naye.

Amedai wataalamu wa simu na kompyuta kutoka Jeshi la Polisi hawakutoa ushahidi mahakamani kuwa baada ya kuchukua simu walizuia vitu kuingia ndani au kutoka nje ya simu hiyo, hivyo ilipoteza sifa ya kuendelea kuwa ushahidi mahakamani hapo.

Amedai mwenye mamlaka ya kuthibitisha kuwa simu inamilikiwa na nani ni kampuni ya mawasiliano ya simu ambayo ilitajwa mahakamani, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na risiti inayoonyesha jina la aliyenunua au boksi la simu.

"Lakini hakuna ushahidi ulioletwa mahakamani ulioonyesha hayo yote, hakuna mwenye mamlaka hata mmoja aliyekuja kutoa ushahidi kuwa simu hiyo ilikuwa ni ya mshtakiwa namba moja, kwa hiyo upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha kosa bila kuacha shaka," amedai.
 
Mmmmmmmhhhhh!!!!! Sheria ishaenda pindishwa hapa ,mbona wakili kaishia tu Kwenye kunywa pombe na kucheza muzikiii....
.VP wakili kitu Cha mpepe a.k.a mmea au mjani ukuona bwana nyundo anavyokipuliza uku akitoa Moshi puani Kwa madaa ,ukuu anamtembezea binti bakoraa...au cku hzi mmea ruksaa wakili

FB_IMG_1748539653564.jpg
 
Ila sheria ni upumbavu ifike mahali watuachie raia tuwe tunamalizana tu wenyewe huku mtaani. Hizi hoja alikuwa wapi kuzisema wakati kesi inaendelea?
 
Raia wakiachiwa wamalizane una uhakika ungekuwa hai hadi mda huu unavyopost jamii forum?
Tungeheshimiana! Hakuna wa kufanya ujinga! Sasa unaona mbinu inayotafutwa hapo? Wameshaona kuna loop hole ya kuwachomoa? Halafu hakuna watu wa hovyo kama wanasheria, wanatoaga rushwa hao ni hatari!
 
Back
Top Bottom