Nyuzi za jf zilizo bora kwangu, zilizowahi kunichekesha sana

Nyuzi za jf zilizo bora kwangu, zilizowahi kunichekesha sana

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Humu jf kuna watu story zao ni zaidi ya movie,

Uzi wa kwanza ni WA huyu jamaa anajiita analyse, title ya Uzi inasema sijivunii mama wa mtoto wangu, jamaa alipigwa na dingi yake kabari sababu ya kuzalisha jimama, jamaa alipigwa kabari hadi akajinyea,😂😂😂 alivoachiliwa akajisemea kichwani akiruhusu dingi yake ampige tena kabari atakunya tena😂😂😂

Uzi mwingine ni WA huyu jamaa namuita Mzee wa U-turn sikumbuki title ya Uzi jamaa alimtongoza mdada co worker, sasa kwenye dates mdada anachagua viwanja kama seacliff, siku wamepanga waende wakalane mdada akaomba wapitie mlimani city jamaa kujihami kumpa mdada elf 40, mdada akamwambia asiwe na haraka, jamaa kwenye shopping alipata mshtuko alivoona dada anachukua kopo la nido la elf 45, pasi, etc jamaa anasema alitokwa na jasho pamoja na ac Kali iliomo kule ndani, jamaa alizima simu akapiga u turn akakimbia, yule mdada😂, kuja kuwasha simu ni sms za matusi za uyo mdada

Uzi Mwingine date ya kwanza mdada alimpeka jamaa kempisiki, wakati jamaa bajet yake mfukoni elf 80, jamaa anasema alihisi tumbo la kuhara baada ya kuona vinywaji tu ni laki Bado msosi, wakati mfukoni ana elf 80 tu, hahaha kumpigia simu rafiki yake aokoe jahazi, rafiki kuja pale ndo kwanza kamuumbua jamaa mbele ya demu kwa kusema siku zote wanagonga bia baa za vichochoroni huko kafata nini😂😂kamaa

Uzi mwingine jamaa alikodi teksi toka korogwe Hadi dar kwenda kumpiga jamaa mlokole aliokuwa anagegeda mke wake 😂

Uzi mwingine mtu alichukua mwanamke kulala nae lodge half kwenye begi kulikuwa na million 5 za kampuni, kufika asubuhi mdada hayupo na million 5 hazipo, anasema alienda chooni alivofika alikojoa bila kulenga tundu, huku akijamba kwa pupa sababu ya uoga😂😂😂😂😂

Long live jf 😂😂😂
 
Visa vingine mbona kama ni vya kutunga tu
 
Huu uzi wa Cosovo ulinichekesha na kusikitisha pia..
👇
 
Sema mkuu Analyse kiboko sana kuna story yake nilikuwa nasoma nacheka mno kama mwehu, kipindi hicho naumwa nikicheka napata maumivu sana ila sikuacha kuisoma. Hongera sana bro una kipaji
 
Huu uzi utacheka ufe...
 
Na ule wakusema tulio wahi kufirisika kuna jamaa anunua pikipiki kwa ajili ya kufaitia demu na mwingine hela za urithi yeye ni kwenda ATM na kutoa mwisho wa siku🤣🤣
 
Back
Top Bottom