Nywele na kitovu cha mtoto hupelekwa wapi?

Nywele na kitovu cha mtoto hupelekwa wapi?

Watu wa pwani wanaoamini katika ushirikina na kuogopa wachawi huwa wanafukia na juu yake wanapanda mti kama muembe

Wengine wanachoma moto na wengine wanatumbukiza chooni

Kama huamini katika mambo ya ushirikina na huwa unamwombea mwanao basi ni unaweza kutupa tu na hakuna kitakachotokea

Kama ni uchawi wa nywele watu wenye saloon na barber shop wangetajirika sana kwsbb unamwachia nywele za kutosha kwake.
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Nywele za watoto wachanga zinaponyolewa huwa zinapelekwa kwa nani na kwanini?

Pia kumekuwa na kitovu cha mtoto kimekuwa kikichukuliwa huwa wanapeleka wapi?

Pia wanaochukua kitovu na nywele wanazifanyia nini?

Haya maswali nimejiuliza ni baada ya kusikia kwa Kuhani Musa katika ibada ya Jumapili ya keo iliyokuwa ikieleza kuhusu nywele na kitovu cha mtoto.

Kuhani Musa yeye anasema kuwa nywele na kitovu cha mtoto huchukuliwa na wachawi kwa lengo la kuharibu akili za watoto na mambo mengi yahusuyo mafanikio ya maisha.

Pia anasema kuwa nywele za wanaume hazipaswi kunyolewa kipara.

Pia wanawake wanapaswa kufunika vichwa vyao wanapofanya ibada.

Nimeona nilete hapa maana kuna watu wa imani mbalimbali ili tujuzane zaidi...

Siku ukija jifungua wa kwako utajua tuu
 
Back
Top Bottom