Siku chache baada ya kufariki nywele za mtu pamoja na kucha zake huonekana zikiwa zimeongezeka urefu.
Jambo hili huonekana mara nyingi sana, linaweza pia kuthibitika kwa kutazama masalia ya binadamu yanayoibuliwa kila kukicha.
Baada ya kufariki, sayansi inasema kuwa ukuaji wa kiumbehai kupitia seli hai zake hufikia mwisho, mifumo yote tendaji hukoma na hakuna jambo lolote ambalo huendelea. Kwanini ukuaji wa sehemu hizi unapingana na sayansi?

- Tunachokijua
- Ngozi na kucha huwa haziendelei kukua baada ya kupatwa na umauti. Hata hivyo, ni muhimu kukubaliana na ukweli kuwa sehemu hizi huonekana zikiwa zinaongezeka urefu tofauti na zilivyokuwa awali.
Mwili hupoteza kiasi kikubwa cha maji baada ya kifo (dehydration), hivyo ngozi huanza kusinyaa na kujivuta (shrinking).
Kusinyaa na kujivuta huku kwa ngozi hufanya kiasi fulani cha kucha na nywele zilizokuwa zimeshikizwa chini yake zijivute kwa nje, hivyo kuonekana zikiwa zimeongezeka urefu kwa kiasi fulani. Huu siyo ukuaji, bali ni ongezeko la urefu linalotokana na kusinyaa kwa ngozi.
Aidha, ukuaji wa kucha na nywele za mwili huhitaji nishati inayozalishwa na glucose ambayo huwa haipo kwa wakati huo.
Pia, kwa mujibu wa Jarida la kitabibu la The BMJ, mfumo unaoratibu ukuaji wa sehemu hizi kupitia vichocheo vya mwili (homoni) husimama baada ya kifo, hivyo hakuna namna yoyote inayoweza kufanya ukuaji huu uendelee.