X men
Member
- Dec 26, 2021
- 18
- 35
Habari wana JF.
Leo napenda kuzungumzia kero ya huduma za Afya katika zahanati nyingi za mkoa wa Tabora.
Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la ufunguzi wa zahanati mpya katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tabora na maalum niizungumzie Halmashauri ya Nzega Vijijini ambayo imefungua zahanati nyingi mpya lakini zina huduma mbovu sana kwakua hizo zahanati zinakua na mtoa huduma mmoja, ikitokea huyu mtoa huduma kapata dharura basi kituo kinafungwa na watu wanakosa huduma.
Kwa sasa wako katika vipindi vya maandalizi ya bajeti ya 2025/26, wananchi tunapata shida kwani muda mwingi zahanati zinafungwa na tunakosa huduma.
Sasa lengo la kufungua zahanati kisha unapeleka mhudumu mmoja ambaye huyo huyo atibu, azalishe na kufanya majukumu ya kiuongozi inawezekana vipi? Si bora wasingezifungua sasa?
Hii ni kero kubwa kwetu wananchi wa Nzega.