Naona kama siasa inaingizwa katika shughuli hii ya kudhibiti nzige. Waziri aliongea kwamba wanapulizia dawa na watakua wamewamaliza nzige wote kwa muda wa siku mbili au tatu tu!
Kwa maoni yangu jambo hili sio jepesi kama inavyoelezwa na wanasiasa. Wenzetu Wakenya wanapambana na makundi ya nzige kwa zaidi ya miezi sita sasa na bado hawajafanikiwa kuwamaliza pamoja na kua wao wana vifaa vya kisasa zaidi kuwasaidia kupambana na mlipuko huo
Ni vizuri Wizara ya Kilimo na Serikali yetu kwa ujumla vifanye juhudi za makusudi kuweka mikakati endelevu ya kupambana na wadudu hawa waharibifu ikiwa ni pamoja na kushirikiana bega kwa bega na wenzetu wa Kenya